Skip to main content

Waziri Mwakyembe ataka mgogoro uishe .!

Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dk Harison Mwakyembe ametoa siku mbili mgogoro baina ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi ili uishe moja kwa moja.

Dk Mwakyembe aliagiza hayo jana nyumbani kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Oysterbay, Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys wanaokwenda Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za Afrika nchini Gabon mwezo ujao.

Mwakyembe amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake akutane na Katibu wa Wizara ya Fedha na kwa pamoja wakakae na Kamishna Jenerali wa TRA ndani ya siku mbili wazungumze na kutatua tatizo hilo. 

"Ikishindikana hiki kikao kufanyika (Mama Samia) nitakuja kushitaki kwako. Hicho kikao naomba kifanyike kama nilivyoagiza mapema, sitaki kusikia tena kuhusu hilo deni,"alisema Dk Mweakyembe na kuongeza;.
"Ninaogopa nisipoyasema haya mapema (TRA), watakuja kukamata basi wakati linakwenda Uwanja wa Ndege tukachelewa ndege ya kwenda Morocco,".

Dk. Mwakyembe alisema anachukua hatua hiyo kwa sababu baada ya kulifuatilia deni lenyewe linaoikabili TFF linaonekana ni la Serikali. 
Kauli ya Dk Mwakyembe ilifuatia TRA kupitia kampuni ya udalali na minada ya Yono kukamata basi la timu ya taifa, Taifa Stars ambalo kwa sasa linatumiwa na timu ya Serengeti Boys.

Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kwamba basi lilichukuliwa katika hoteli ya Urbun Rose, Kisutu, Dar es Salaam likiwa linawasubiri wachezaji wa Serengeti Boys liwapeleke kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

Hatua hii inakuja kiasi cha wiki tatu baada ya TRA kupitia Yono pia kuzifunga ofisi za TFF kutokana na deni kubwa la kodi na la muda mrefu.Deni hilo la Sh. Bilioni 1.2 linatokana na kodi za mishahara ya waliokuwa makocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo na Mdenmark, Jan Borge Poulsen kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.

Tayari TFF chini ya Rais wake, Jamal Malinzi imefanikiwa kulipa deni lingine la zaidi ya Sh. Milioni 400 kodi ya Ongezeko la Thamani (VaT) la ziara ya timu ya taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njiani kwenye Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia.BBC

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...