Skip to main content

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa.

Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo.

Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo.

Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii.

Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo
Marekani, Ufaransa na Uingereza zimewasilisha rasimu ya azimio kwa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa likishutumu mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu hapo Jumanne katika mji unaoshikiliwa na waasi kaskazini magharibi ya Syria na kudai yafanyiwe uchunguzi.

Azimio la kurasa mbili ambalo shirika la habari la Ujerumani dpa lilipata nakala yake limetaka lipatiwe taarifa za kina juu ya operesheni za anga za ndege za jeshi la Syria na majina ya marubani wa helikopta za serikali.

 Shirika la Kupiga Marufuku Matumizi ya Silaha za Sumu limetaka lipatiwe nafasi ya kuzuru viwanja vya ndege vya kijeshi ambapo inadaiwa silaha hizo za sumu zilifyatuliwa.

Limetaka kukutana na majenerali wa Syria na viongozi wa Syria katika kipindi kisichozidi siku tano. Akizungumza hapo jana katika mkutano na waandishi wa habari msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujaric amesema Umoja wa Mataifa haukuthibitisha repoti za kutumika kwa silaha za sumu nchini Syria.

Utawala wa Assad umekuwa ukituhumiwa kutumia silaha za sumu mara kadhaa tokea vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza mwaka 2011 yakiwemo mashambulizi katika eneo la Ghouta karibu na mji mkuu wa Damascus kwa kutumia kemikali ya sumu ya sarin ambapo zaidi ya watu 1,400 walikufa katika shambulio la mwaka 2013.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson, amesema kwamba ushahidi wote wa mashambulio hayo ya sumu hadi sasa unaashiria kwamba ni serikali ya Assad iliyotenda hayo kwa kutambuwa fika kwamba inatumia silaha zilizopigwa marufuku kwa mashambulizi hayo ya kinyama dhidi ya wanachi wake wenyewe.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wakaazi wa mji huo unaoshikiliwa na waasi wameathirika kutokana na kushambuliwa kwa kiwanda cha silaha za sumu cha waasi.

Nchi zote mbili, Urusi na Syria, zimekanusha kufanya mashambulizi ya silaha za sumu.
                 Wafadhili wa kimataifa wanatafuta michango ya mabilioni ya dola kuisaidia Syria, nchi iliyoathirika na vita.DW BORN.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...