Skip to main content

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA BASI LA DORTMUND MBARONI UJERUMANI.! Bofya picha hii.

Polisi ya Ujerumani imemtia mbaroni mwanamme Mjerumani mwenye asili ya Urusi,
 anayeshukiwa kufanya mashambulizi dhidi ya basi lililokuwa likiwasafirisha wachezaji wa klabu ya Borussia Dortmund wiki iliyopita.

Makomando wa polisi ya Ujerumani, kwa niaba ya ofisi mwendesha mashitaka wa shirikisho wamemkamata mtuhumiwa huyo, 
mwenye umri wa miaka 28 katika mji wa Tübingen katika jimbo la Kusini Magharibi mwa Ujerumani la Baden Württenberg.

Taarifa za awali kutokana na uchunguzi uliofanywa zimeonyesha kuwa mshambuliaji huyo aliyetambulishwa kwa jina la Sergej W.

alitaka kunufaika na kuanguka kwa thamani ya hisa za klabu ya Borussia Dortmund, ambako alitarajia kungetokana na taarifa za mashambulizi kwenye basi iliyobeba wachezaji wa klabu hiyo.

Uchunguzi umebainisha kuwa Sergej alikuwa amenunua hisa za klabu hiyo zenye thamani ya euro 78,000 kupitia mtandaoni,
 akiwa katika hoteli ya klabu hiyo alikokuwa amekodi chumba kuanzia tarehe 9 mwezi huu wa Aprili. 

Miripuko mitatu ilitokea karibu na basi la Borussia Dortmund siku mbili baadaye, tarehe 11 Aprili wakati wachezaji walipokuwa wakienda kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, dhidi ya timu ya AS Monaco ya Ufaransa.
Screenshot Instagram Marc Bartra 12.4.2017 (Instagram/marcbartra) Marc Bartra, mchezaji aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo
Mchezaji mmoja wa Dortmund, 
mhispania Marc Bartra alivunjika mkono katika shambulizi hilo, na mechi hiyo iliahirishwa hadi siku iliyofuata.

 Hali kadhalika, afisa wa polisi aliyekuwa akiendesha pikipiki kusindikiza basi hilo la wachezaji, alipata mfadhaiko kutokana na kelele za miripuko.

Taarifa za uchunguzi zimesema katika ununuzi wa hisa za klabu ya Dortmund, mshukiwa alikuwa amejiwekea uwezekano wa kuziuza tena hisa hizo kwa bei iliyotangazwa kabla, na kulingana na utaratibu wa soko la fedha, 
kuanguka kwa kiasi kikubwa kwa thamani ya hisa za klabu ya Borussia Dortmund kungempatia faida ambayo ni zaidi ya mara kadhaa ya mtaji aliokuwa ameuwekeza.

Ofisi ya mwendesha mashitaka iliyoitoa ripoti hiyo, imesema iwapo kungetokea vifo vya wachezaji katika shambulizi hilo, thamani ya Dortmund ingeporomoka kwa kiwango kikubwa.

Mashitaka anayokabiliwa nayo mshukiwa huyo ni pamoja na jaribio la kuuwa, kusababisha madhara makubwa ya kimwili kwa wahanga, na pia kusababisha mripuko.

Polisi walitilia shaka ujumbe ulioachwa eneo la tukio kuashiria kuhusika kwa IS
Awali shambulizi hilo lilikuwa likushukiwa kuwa la kigaidi,

kutokana na kikaratasi kilichookotwa eneo la shambulio, 
kikidai kuandikwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS likikiri kuhusika na miripuko hiyo. 

Hata hivyo polisi mara moja walitilia shaka ukweli wa ujumbe huo.
Usalama ni suala nyeti nchini Ujerumani wakati huu wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho utakaofanyika mwezi Septemba, 
ambamo azma ya Kansela Angela Merkel kuwania mhula wa nne inakabiliwa na ushindani mkubwa.

Mwaka jana chama cha Bi Merkel kilipoteza uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa, kutokana na sera yake ya kuwafungulia milango wakimbizi zaidi ya milioni moja.

Wasiwasi ulizidi kuongezeka baada ya shambulizi lililofanywa na kijana kutoka Tunisia dhidi ya soko la Krismasi mwaka jana mjini Berlin, ambalo liliuwa watu 12 na kuwajeruhi wengi wengine.DW

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...