Marekani imefanya shambulizi la makombora takriban 50 ,yalipigwa katika kambi ya jeshi la anga mjini Homs nchini Syria.
Awali
maafisa wa Marekani walisema wana mpango wa kuchukua hatua za kijeshi
baada ya Syria kushutumiwa kutumia silaha za kemikali katika mji
unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha.
Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea. Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameamuru
kutekelezwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria huku akitoa wito
kwa mataifa yote yaliyostaarabika kukomesha vitendo vya mauaji na
umwagaji damu nchini humo
Naye mshirika wa Syria Urusi
ametahadharisha madhara yatokanayo na hatua zozote za kijeshi
zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria . Hata hivyo Rais Donald Trump amsema kuwa ,kutumia gesi hatari kuua
raia wakiwemo watoto wengi, utawala wa Syria ulikuwa umevuka mipaka. Mike Pregent ni mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati ameiambia BBC kuwa mashambulizi hayo yametoa ujumbe mzito kwa Assad.
Shambulio
hilo linawapa Watu wa Syria matumain, na ninachomaanisha ni kuwa haya
hakika haya ni Mashambulizi dhidi ya vikosi vya anga vya Assad, silaha
za kemikali, pengine dhidi ya hifadhi za mafuta halikadhalika.hivyo
haikuwa dhidi ya raia, haikuwaweka marubani wa kimarekani hatarini.
Ulikuwa ujumbe maalum kwa Assad kuwa usitumie jeshi lako la anga
kuwaadhibu raia, hivyo nafikiri ni ujumbe wenye nguvu.BBC
Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani. Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...
Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...
Comments
Post a Comment