Wahudumua wa ndege ya shirika la
ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani
umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua
mtoto msichana.
Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.
Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini.
Mashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.BBC
Comments
Post a Comment