Wasafiri katika mji mkuu wa Uingereza London, hivi karibuni wataanza kutumia magari ya usafiri yasiyo na dereva.
Magari hayo ambayo husafiri kwa hadi kasi ya kilomia 16.1 kwa saa, yataelekezwa na kompyuta.
Hata hivyo kutakuwa na mtu ndani ya gari hilo ambaye anaweze kulisimamisha ikiwa itahitajika.

Magari hayo yanawabeba watu wanne na hayana usukani wala breki,
Gari hilo lina kamera ambayo inaweza kuona umbali wa mita 100 na husimama wakati kuna kitu chochote mbele yake.
Maafisa wa mradi huo wanaamini kuwa magari hayo, yatasaidia katika kuboresha usafiri eneo la Greenwish jijini London.BBC
Comments
Post a Comment