Skip to main content

MZOZO WA KIVITA KATI YA KOREA YA KASKAZINI NA MAREKANI WAZIDI KUPAMBA MOTO.! Bofya pich hii...

Mzozo kati ya Marekani na Korea ya kaskazini unazidi makali. Jamhuri ya umma wa china inaonya mzozo huo unaweza kuripuka wakati wowote ule na hakuna atakaeibuka na ushindi.

Onyo la waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Wang Yi limefuatia vitisho vya rais wa arekani Donald Trump dhidi ya utawala wa mjini Pyongyang."

Majadiliano ndio njia pekee ya kupatikana ufumbuzi" amesema waziri Wang katika mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mwenzake wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema "mzozo wa Korea ya kaskazini utashughulikiwa."

Yeyote atakaesababisha mzozo katika rasi ya Korea "atabeba jukumu la kihistoria la yatakayotokea" ameshadidia waziri wa mambo ya nchi za nje wa China. 

Katika kadhia ya mradi wa nuklia wa Korea ya kaskazini,"Mshindi hatokuwa yule mwenye kutoa maneno makali au anaetaka kuonyesha misuli".

Vita vikiripuka, matokeo yake yatakuwa kuibuka hali ambayo hakuna atakaejiita mshindi" ameonya waziri Wang. Jamhuri ya umma wa China,inayoangaliwa kama mshirika pekee wa Korea ya kaskazini,
inapinga mradi wa nuklea wa utawala wa Kim Jong Un, hata hivyo kila mara imekuwa ikiisihi Marekani ijizuwie.


Kwa mujibu wa wadadisi, Korea ya kaskazini inaweza kufanya jaribio jengine la kombora la nuklea kesho itakapoadhimisha miaka 105 ya kuzaliwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo Kim Il Sung.
"Hatua za kijeshi zinazingatiwa" amesema mshauri wa masuala ya kisiasa wa ikulu ya Marekani ambae hakutaja jina lake litajwe na kuongeza anaamini Pyong yang itafanya jaribio jengine ama la kombora alinaloweza kupiga toka bara moja hadi jengine,au la kinuklea.

 Jumamosi iliyopita rais wa Marekani ameamuru manuari inayobeba ndege za kivita Carl Vinson iliyosindikizwa na manuari nyengine tatu zilizosheheni mitambo ya kufyetulia makombora na 
 nyambizi kadhaa zielekee katika raas ya Korea.
 

Wakati huo huo makamo wa rais wa Marekani Mike Pence anatarajiwa kuwasilio Korea ya kusini jumapili hii,akianza ziara ya siku kumi katika nchi za Asia Pacific.

 Mzozo wa Korea ya kaskazini ndio mada kuu atakayoizungumzia atakapokutana na viongozi wa Korea ya Kusini, Japan, Indonesia na Australia.DW BORN.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...