Skip to main content

Ujerumani, Poland na England zajiimarisha.!

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw alikamilisha kazi yake baada ya mabingwa hao wa dunia kupata ushindi watano kwenye mechi tano katika Kundi lao la kufuzu Kombe la Dunia.

Ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Azerbaijan mjini Baku ulikuwa suala rahisi tu kwa Wajerumani ambao walifungwa bao lao la kwanza kabisa katika Kundi C.

 Ujerumani wanaongoza kileleni na pengo la pointi tano dhidi ya Ireland ya Kaskazini ambayo iliizaba Norway 2-0. 
Nayo Jamhuri ya Czech iliizaba San Marino 6-0.

England ilipambana na kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Lithuania. Ni mechi ambayo mshambuliaji Jermain Defoe mwenye umri wa miaka 34 alirejeshwa kikosini na akafunga bao lake la 20 la kimataifa.

 England sasa imejiimarisha kileleni mwa Kundi F. Vijana hao wa kocha Garry Southgate sasa ndio timu pekee ya Ulaya ambayo haijafungwa bao hata moja kufikia sasa. 

England wana pointi 13, nne mbele ya Slovakia ambao walisonga katika nafasi ya pili ya kundi hilo kwa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Malta. Scotland wako nyuma na pengo la pointi sita baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovenia.


Katika Kundi E, nahodha wa Poland Robert Lewandowski alifunga bao katika mechi ya kumi mfululizo na kuiweka kileleni timu yake kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Montenegro. 

Montenegro sasa iko na pointi saba sawa na Denmark baada ya Wadenmark kutoka sare tasa na Romania, ambayo ina pointi sawa na Armenia. Armenia iliifunga Kazakhstan 2-0 na kuyaweka hai matumaini ya kucheza mechi za mchujo.DW BORN

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...