Meneja wa timu ya Manchester United
Jose Mourinho amesema kuwa Luke Shaw alitumia mwili wake lakini ubongo
wa Mourinho wakati wa mechi kati ya Manchester United na Everton, ambayo
iliisha kwa sare ya 1-1.
"Alikuwa mbele yangu na nilikuwa nikimfanyia kila uamuzi" Mourninho alieleza.
Shaw ndiye alikuwa mchezaji mdogo pekee kutoka Manchester aliyetengwa kando na Mourinho baada ya United ilitoka bao sare kwa mara ya tisa nyumbani katika ligi msimu huu.
United ilimshukuru Ibrahimovic tena kwa penalty aliyoufunga iliyosaidia United kupata alama moja na kuiweka United nambari tano kwa jedwali.
Ibrahimovic ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu bado hajaamua iwapo atasalia kubaki Old Trafford msimu ujao.
"Bado tunajadiliana, tungoje kuona matokeo, bado nipo wazi na hakuna lolote limetendeka bado", Ibrahimovic ambaye ana miaka 35 alieleza kupitia televisheni ya manchester united.
"Nilikuja hapa bila Ligi ya Mabingwa, haikuwa timu ambayo ilitarajiwa kushinda, lakini bado nilikuja na nikasaidia nilivyoweza ili kuiimarisha, kwa hivyo tungojee kuona matokeo.BBC
Comments
Post a Comment