Saudi Arabia imeanzisha mipango ya
kujenga mji wa burudani kando mwa mji wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa
mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya Gibraltar.
Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani.
Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022.
Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin Salman mwaka mmoja ulipita,
una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia kutegemea mafuta kwa taifa hilo.
Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa.
Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh.BBC
Comments
Post a Comment