Leo
September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali
Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Posta Tanzania.
Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016. Luteni
Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi
na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo,
Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe
05 Septemba, 2016. Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais
Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016. Dkt. Hedwiga Francis Swai ni
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016. Balozi
Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi
Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.
Aidha, Rais
Magufuli amemteua Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume
ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016 Fidelis
Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF.Chanzo Mpekuzi.

Comments
Post a Comment