Skip to main content

Waziri Mkuu Majaliwa atoa wiki moja kwa Afisa Elimu kutafuta walimu wa kidato cha tano na sita.......//

WAZIRI MKUUkuu  Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji. 
 
Ametoa agizo hilo  Jumatatu, Septemba 26, 2016  wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.  baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule. 
 
"Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri Mkuu. 
 
Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira. 
 
 "Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa. 
 
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa. 
 
 Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria. 
 
 "Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu. 
 
 Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi. 
 
 Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini. 
 
 Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua. 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...