Skip to main content

Watoto 2,570 waripotiwa kulawitiwa kwa kipindi cha miezi saba...............///

Vitendo vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi nchini katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambapo zaidi ya watoto 2,570 wa kike na kiume wamelawitiwa na kubakwa.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yaliyofanyika jana katika Makao makuu ya watoto yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Helen Kijo-Bisimba alisema idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na ya mwaka jana.

Hata hivyo, Mama Bisimba alisema kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, takwimu hizo zinaweza kuwa ndogo kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ulawiti kwa watoto kutoripotiwa polisi kwa sababu ya mila na desturi za maeneo mengi nchini.

“Ripoti ya Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kati ya Januari na Machi 2016 inaonyesha matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa yakiendelea kuongezeka kutoka 180 hadi 1765 hayo ni matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo mbalimbali vya polisi nchi nzima ukilinganisha na matukio 1585 mwaka 2015. Hata hivyo waliohusika na matukio hayo wameonekana wakirandaranda bila kuchukuliwa hatua za kisheria, ”alisema.

Alisema ripoti hiyo inaonyesha kuwa kesi 1,203 zipo katika hatua ya upelelezi, 822 zipo mahakamani na watuhumiwa 234 wamekwisha hukumiwa.

“Pia utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto kwa kushirikiana na Tanzania kitengo cha ustawi wa jamii unaonyesha kati ya watoto 10 wa kike 4 wamebakwa, na kati ya watoto 10 wa kiume 3 wamelawitiwa zaidi ya mara tatu. Utafiti huo unaonyesha kwa ujumla kuwa watoto wa kike na wa kiume 6 walifanyiwa ukatili huo na watu ndani ya familia,” alisema.

Bisimba alisema asilimia 49 ya ukatili hufanyika nyumbani, 23 hufanyika njiani wakati wa kwenda shule au kurudi, na asilimia 15 hufanyika shuleni. Pia ripoti hiyo ya UNICEF inaonyeaha kuwepo kwa matukio ya watoto kulawitiana na kubakana wenyewe kwa wenyewe kutokana na kuvizoea vitendo hivyo.

LHRC imeitaka serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto na kutilia mkazo malezi bora kwa watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakachotoa adhabu kali kwa familia itakayoshindwa kutoa malezi bora kwa mtoto.

LHRC inayoshughulika na utetezi wa sheria na haki za binadamu ilianzishwa Septemba 26, 1995.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...