Wiki iliyopita Ikulu ya Nigeria kupitia kwa muandishi wa hotuba za Rais, iliingia kwenye skendo ya kunakili hotuba ya Rais Barack Obama na kumpa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye aliisoma kama ilivyo bila kujua, mpaka wapinzani walipoanzisha mzozo juu ya suala hilo.
Sehemu ya hotuba ya Rais Buhari iliyonakiliwa kutoka kwenye hotuba ya Rais Barack Obama aliyoitoa mwaka 2008 inasema “Change Begins With Me” Mabadiliko Huanza Na Mimi, ikifahamika kwa jina la Hotuba ya Ushindi.
Ikulu ya
Nigeria imeomba radhi juu ya aibu iliyomkuta Rais wa nchi hiyo na
kuahidi kumchukulia hatua kali za kinidhamu muandishi aliyesababisha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Trust
limesema kuwa kiongozi huyo msaidizi wa idara ya mawasiliano ya Rais,
ataondolewa kazini kutokana na uzembe alioufanya. Muda mfupi tangu kutokea
tatizo hilo, Taasisi ya Rais kupitia idara ya mawasiliano kwa Umma
imeripoti kuwa itaweka software itakayokuwa ikigundua kama hotuba zote
za Rais zimenakiliwa kutoka sehemu nyingine.
Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema >>>Tumepanga
kuchukua hatua ya kuweka kifaa kitakachokuwa na uwezo wa kukagua na
kugundua kama hotuba za Rais zimenakiliwa kutoka sehemu nyingine kabla
ya kumkabidhi Rais,”
Kitendo
cha Hotuba ya Rais Buhari kunakiliwa kutoka kwenye Hotuba za Rais Obama,
kimewafanya vyama vya upinzani nchini humo kusema kuwa ipo siku Rais
huyo atasaini nakala za kujiuzulu bila kujua kutokana na kutozikagua
kabla ya kuzisoma.Chanzo MIlad Ayo
Comments
Post a Comment