Kituo
cha Runinga kinachozidi kufanya vema kwa kasi chaAzam TV, jana Jumnne
kimezundua promosheni yake mpya ya Full Dowzii Kutwa Mara Tatu ambayo
itakuwa mahususi kwa ajili ya wateja wao wapya.
Katika
promosheni hiyo, mteja atapewa king’amuzi, dishi, rimoti na vifaa vyake
vyote pamoja na kuunganishiwa king’amuzi hicho endapo mteja huyo
atalipia kifurushi kikubwa cha Azam Play kwa mwaka mmoja.
Mkurugenzi
wa Matukio wa Azam TV, Yahya Mohamed, amesema: “kwa kawaida mteja mpya
hununua king’amuzi cha Azam TV pamoja na vifaa vyake vyote kwa Sh
135,000, huku gharama za ufundi zikiwa ni Sh 30,000 ambapo jumla ni Sh
165,000.
“Lakini
mteja mpya ukilipia Sh 336,000 kwa ajili ya kifurushi cha Azam Play kwa
mwaka, utaokoa Sh 165,000. Hivyo niwaambie tu wateja wetu Azam tumekuja
kwa ajili ya kuwakomboa na kupata burudani kila siku bila ya kikomo.”
Aidha,
Mohamed alisema, Azam TV ina vifurushi vitatu vya mwezi ambavyo ni Azam
Pure Sh 15,000, Azam Plus Sh 23,000 na Azam Play Sh 28,000 ambapo
kifurushi hicho kikubwa ndicho kinachohusishwa na promosheni hiyo.
Comments
Post a Comment