Skip to main content

MAMBO MATATU YALIYOSABABISHA BRAVO KUHAMA FC BARCELONA


Bravo
Na Athumani Adam
Claudio Bravo amekuwa mchezaji wa nane kusajiliwa na kocha Pep Guardiola ndani ya klabu ya Manchester City. Uhamisho wa golikipa huyo raia wa Chile kutoka klabu ya FC Barcelona ni ishara kwamba ule ufalme wa kipa namba moja wa City Joe Hart umefika ukingoni pale Etihad.
Japokuwa uwezo wa Bravo kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma  ndio sababu iliyomvutia Guardiola kufanya usajili huu, makala hii inakupa sababu tatu ambazo zimechangia Bravo kuondoka Fc Barcelona baada ya uchunguzi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika duniani
  1. MSHAHARA MDOGO UWEZO MKUBWA
Kwenye dirisha hili la usajili Barcelona walikuwa na mpango wa kumuongezea Claudio Bravo mkataba kabla ya ule wa awali ambao ulitarajiwa kumaliza mwaka 2018.  Bravo alitegemea mkataba wa kuanzia miaka miwili pia kuongezewa mshahara wa mwishoni mwa wiki.
Barcelona walishindwa kufikia matarajio ya Bravo pale walipoleta mkataba wa mwaka mmoja pamoja na mshahara ambao haukufika kiwango alichokita Bravo. Hadi anaondoka kwenye klabu ya Barcelona  Bravo alikuwa anapokea mshahara wa Euro 33,500 kwa wiki huku golikipa namba mbili Marc Andre Stegen analipwa Euro 55,000 kwa wiki.
  1. BIFU NA MARC ANDRE TER STEGEN
Kauli za Kipa Marc Andre Ter Stegen dhidi ya Bravo zimechangia kuleta bifu la chinichini baina yao. Mara kwa mara Ter Stegen amekuwa akitoa kauli kuwa anataka apewe nafasi ya kucheza hususani kwenye La Liga la sivyo ataihama klabu hiyo zimekuwa hazimvutii Claudio Bravo.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amekuwa akimpa nafasi zaidi ya kucheza Claudio Bravo ukilinganisha na Mjerumani Ter Stegen.
  1. USHAWISHI WA FAMILIA
Bravo na mkewe Carla Pardo walikuwa na mipango ya kuhamia England. Hata watoto wao kule nchini Spain kwenye jiji la San Sebastian wanasoma shule zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza. Hivyo uhamisho huu kwa Bravo hautakuwa na athari yeyote kwenye familia yake

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...