Skip to main content

SUMATRA KUPAMBANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA YA BAHARI.....................///

 Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga jana  kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud
  Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa jana na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
 Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari jana
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA)Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga  
MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.
Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.
Ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.
Aidha alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa mazingira uliopitiliza unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua samaki katika bahari na viumbe vingine vilivyomo baharini.
Alisema Tanzania imeingia katika shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya bahari hali ambayo inalazimika kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda
mazingira ya bahari.
“Hakuna vyombo vinavyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya baharini hivyo imetulazimu kuanzisha mpango maalumu ambao tunategemea kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na
uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.
 Hamza alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya maadhimisho hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia katika mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya usafirishaji wa Majini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho hayo lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani na nje ya nchi.
Alisema Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu ya kitovu cha biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari na hata nchi kavu ikiwa itawekewa mipango madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha  (P.T).Mbotera.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...