Skip to main content

WAASI WA FARC KUSAINI MAKUBALIANO YA AMANI

Colombia itapiga hatua kubwa kuelekea kuliepuka jinamizi la muda mrefu la machafuko wakati serikali na kundi la waasi nchini humo watakaposaini mkataba wa amani uliopatikana baada ya miaka minne migumu ya mazungumzo
Umuhimu wa muafaka huo ni mkubwa mno: mgogoro wa Colombia uliodumu kwa zaidi ya miongo mitano, kwa sehemu ukichochewa na biashara ya dawa za kulevya aina ya cocaine, umeua zaidi ya watu 220,000 na kuwaacha wengine milioni 8 bila makaazi. Ili kuonyesha umuhimu wa siku hii, mkataba huo utasainiwa na Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kamanda mkuu wa Revolutionary Armed Forces of Colombia – FARC, mpiganaji muasi anayefahamika kwa jina la utani la Timochenko. Akizungumza katika mkesha wa siku hii, Rais Santos amesema "Nadhani juhudi zote zilikuwa muhimu na sasa tunastahili kufanya juhudi kubwa zaidi ili kuufanikisha mkataba huu kwa sababu hatuna kikwazo mbele yetu. Natumai kwa pamoja, sote, yani wale wanaounga mkono kura ya "Ndiyo" na wale wenye wasiwasi..kuwa tunaweza kuungana baada ya kura ya maoni kupita na tunaweza kuitengeneza nchi mpya pamoja".
Marais 15 wa Amerika Kusini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry wanatarajiwa kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika mji wa kikoloni wa Cartagena.
Zaidi ya wageni 2,500 walioalikwa kwenye sherehe hiyo wametakiwa kuvalia nguo nyeupe kama ishara ya amani, na Santos atautia saini mkataba huo wa kurasa 297 kwa kutumia kalamu iliyotengenezwa na ganda lililotumika vitani.
Kutiwa saini mkataba huo hakutakuwa mwisho wa mambo hata hivyo. Wacolombia wanapewa fursa ya kuwa na usemi wa mwisho wa kuidhinisha au kupinga mkataba huo katika kura ya maoni ya Oktoba 2. Uchunguzi wa maoni unaonyesha ushindi wa kura ya "ndiyo”, lakini baadhi ya wachambuzi wanaonya kuwa idadi ndogo ya wapiga kura huenda ukawa habari mbaya kwa changamoto nyingi zinazoikabili nchi hiyo katika utekelezaji wa muafaka huo muhimu.
Miongoni mwa hatua kubwa na zenye utata zaidi itakuwa ni kuzifungua kesi za uhalifu wa kivita dhidi ya waasi na wahusika wa serikali. Chini ya kanuni za mkataba huo, waasi watakaoweka chini silaha zao na kukiri makosa yao watasamehewa kifungo cha jela na kutakiwa kuwafidia waathiriwa kwa kufanya kazi ya maendeleo katika maeneo yaliyoathirika pakubwa na mgogoro huo.


Serikali pia imeahidi kushughulikia suala la ugawaji usiokuwa wa usawa wa mashamba, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likizungumziwa na FARC tangu kundi hilo lilipoanzishwa kama jeshi la wakulima wadogowadogo mwaka wa 1964, na serikali ilikubali kushirikiana na waasi ili kuwapa maendeleo mbadala maelfu ya familia zinazotegemea biashara ya cocaine. Kama mkataba huo utaidhinishwa na kura ya maoni, basi wapiganaji karibu 7,000 wa FARC wataanza kuhamishwa hadi maeneo 28 katika kipindi cha miezi sita ijayo ambapo watasalimisha silaha zao kwa waangalizi watakaosimamiwa na Umoja wa Mataifa. DW

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...