Skip to main content

MAREKANI: IRAN INAFANYA UCHOKOZI WA HALI YA JUU.!

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameituhumu Iran kwa kufanya "uchokozi wa hali ya juu" unaoendelea ambao amesema unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika kanda hiyo.

"Iran isipochukuliwa hatua inaweza kwenda njia sawa na ya Korea Kaskazini na kuubeba ulimwengu wote katika safari hiyo," Bw Tillerson amesema.

Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Hata hivyo, Marekani imekiri kwamba Tehran inatii makubaliano hayo ya mwaka 2015.
Iran kufikia sasa haijasema lolote kuhusu tamko hilo jipya kutoka kwa Marekani.

Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia.

Jumanne, Marekani iliituhumu Korea Kaskazini na kusema taifa hilo lilikuwa linajaribu kufanya "uchokozi kutokee jambo fulani", baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki.

Kuijibu Marekani, Korea Kaskazini ilisema inaweza kuwa ikifanya majaribio ya makombora kila wiki.

Aidha, ilionya kwamba itaikabili Marekani kwa vita vikali iwapo taifa hilo litathubutu kuishambulia kijeshi.

'Vitisho vingi'

Jumatano, Bw Tillerson alsiema utathmini huo mpya kuhusu Iran, ambao aliutangaza katika Bungela Congress siku moja awali, 

kando na kutathmini iwapo Tehran imetimiza makubaliano ya mkataba huo wa nyuklia pia utachunguza vitendo vya Iran Mashariki ya Kati.

Bw Tillerson aliituhumu Iran kwa kuhujumu juhudi za Marekani nchini Lebanon, Iraq, Syria na Yemen. 

"Mpango wa kina wa sera kuhusu Iran unatuhitaji tuangazie vitisho hivi vinavyoletwa na Iran, na ni wazi kwamba ni vingi (vitisho)," alisema.
Bw Tillerson awali alikiri kwamba Iran ilikuwa imeheshimu makubaliano ya mkataba huo wa 2015, lakini aliibua wasiwasi kuhusu taifa hilo akisema limeendelea kuwa "mfadhili wa ugaidi".

Rais Trump kwa muda mrefu amekuwa akisema mkataba huo kuhusu Iran "ndio mbaya zaidi kuwahi kutiwa saini".

Hata hivyo, mtangulizi wake Barack Obama alisema mkataba huo, kati ya Iran na mataifa sita yenye ushawishi duniani zikiwemo China, urusi na Uingereza,
 ilikuwa ndiyo njia bora zaidi ya kuizuia Iran kustawisha silaha za nyuklia.BBC

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...