Skip to main content

Taarifa ya Abdi Banda kusimamishwa kucheza ligi kuu Tanzania bara.!

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, ilifanya kikao chake juzi Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao.

Kuhusu kupulizwa dawa vyumbani Uwanja wa Kambarage
Daktari wa Uwanja wa Kambarage, Dk. 

Abel Kimuntu amekataa kuwasilisha taarifa yake kuhusu tuhuma za kupuliziwa dawa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Majimaji katika mechi namba 170 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji Stand United.

 Klabu ya Majimaji iliwasilisha malalamiko yake kwa Bodi ya Ligi kuhusu suala hilo.
Hivyo, Kamati imeagiza suala la daktari huyo lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya hatua za kinidhamu dhidi yake kutokana na kukataa kutoa ushirikiano kwa mwendeshaji wa Ligi juu ya jambo hilo. Kamati ya Nidhamu inatarajiwa kukaa wakati wowote wiki ijayo.

Kuhusu Mchezaji Abdi Banda
Mechi namba 194 (Kagera Sugar 2 vs Simba 1). Beki wa Simba, Abdi Banda jezi namba 24 amesimamishwa kucheza Ligi Kuu wakati akisubiri suala lake la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla jezi namba 15 wakati akiwa hana mpira kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Alifanya kitendo hicho ambacho hakikuonwa na waamuzi katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 2, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
Pia Kamati ilibaini kuwa Banda alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote.

Kwa vile kosa hilo ni la kinidhamu, Kamati imemsimamisha Abdi Banda kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) wakati akisubiri suala lake kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Kamati ya Nidhamu inatarajiwa kukaa wakati wowote wiki ijayo.

Kadhalika Klabu ya Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na timu ya Kagera Sugar kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi Gharib wakati akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 2, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kamati baada ya kupitia malalamiko hayo, imeahirisha shauri hilo hadi Alhamisi Aprili 13, 2017 kwa vile bado inafuatilia baadhi ya vielelezo kuhusu malalamiko hayo kabla ya kufanya uamuzi.

Mechi namba 195 (Yanga 1 vs Azam 0). Yanga haikuingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo, kutokana na kuwa na maji yaliyomwagwa na wanachama wa klabu hiyo (makomandoo) muda mfupi kabla ya timu hiyo kuwasili uwanjani.

Kamati imeelekeza klabu ya Yanga iandikiwe barua ya onyo, na kuitaka kuhakikisha wanachama wake wanaacha mara moja mtindo wa kumwaga maji vyumbani baada ya kuwa vimeshafanyiwa usafi na wafanyakazi wa uwanja tayari kwa ajili ya matumizi ya timu yao.
Mechi namba 200 (Majimaji 4 vs Toto Africans 1). Katika mechi hiyo, timu ya Toto Africans ilifanyiwa vurugu ikiwa njiani kurejea hotelini baada ya mechi hiyo ambapo viongozi wake wawili waliumizwa. Tukio hilo liliripotiwa Kituo cha Polisi, na kesi tayari iko kortini.
Kituo cha Songea (Uwanja wa Majimaji) kiandikiwe barua ya kuhakikisha hazitokei vurugu uwanjani hapo baada ya mechi ikiwemo kuhakikisha timu ngeni inatoka uwanjani salama hadi kwenye hoteli ilikofikia. 

Iwapo vurugu zitaendelea, Bodi ya Ligi itasimamisha matumizi ya kituo hicho kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 9(2) ya Ligi Kuu.DAUDA

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...