Skip to main content

MAHAKAMA NCHINI URUSI YAPIGA MARUFUKU MASHAHIDI WA YEHOVA.!

Mahakama ya Juu nchini Urusi imekubali ombi la serikali kuorodhesha kanisa la Mashahidi wa Yehova, kwa Kiingereza Jehovah's Witnesses,
 kama kudi la kidini lililoharamishwa, na kuliorodhesha kuwa kundi lenye msimamo mkali.

Wizara ya haki nchini humo ilisema kundi hilo lilikuwa limesambaza nyaraka zilizokuwa na ujumbe wa kuchochea chuki dhidi ya makundi mengine.

Mawakili waliokuwa wanatetea kundi hilo wamekanusha madai hayo na wamesema watakata rufaa.

Kundi hilo la kidini lina waumini 175,000 nchini urusi, taifa ambalo wafuasi wa madhehebu hayo waliteswa na kudhulumiwa wakati wa utawala wa Josef Stalin.

Inakadiriwa kwamba kuna watu milioni nane kote duniani ambao ni waumini wa madhehebu hayo ya Kikristo, yanayofahamika sana kwa kampeni zake za kwenda nyumba kwa nyumba kutafuta waumini wapya.

Wafuasi wa kundi hilo la kidini wanasema hatua ya kuharamisha kundi hilo ina maana kwamba shughuli zake pia ni haramu kisheria.

Wizara ya haki iliiomba mahakama kufunga makao makuu ya kitaifa ya kundi hilo la kidini karibu na mji wa St Petersburg, 

mashirika ya habari ya Urusi yalisema, pamoja na kupiga marufuku baadhi ya vitabu vyenye msimamo mkali vinavyochapishwa na kundi hilo.
Moja ya vijitabu vilivyosambazwa na kundi hilo nchini Urusi vilimnukuu mwandishi mashuhuri wa vitabu Leo Tolstoy akieleza imani kuu ya kanisa la Orthodox la Urusi kama ushirikina na uchawi.

maafisa wamelituhumu kundi hilo la kidini kwa kuharibu familia, kupanda mbegu za chuki na kuhatarisha maisha.

mashahidi wa Yehova wanasema tuhuma hizo si za kweli.
Msemaji wa kundi hilo aliambia shirika la habari la AFP kwamba alishangazwa sana na uamuzi huo.

"Sikutarajia kwamba hilo linaweza kutokea katika Urusi ya sasa, ambapo katiba inawahakikishia raia uhuru wa kuabudu," alisema Yaroslav Sivulsky.
Image caption Urusi imesema vitabu vya Mashahidi wa Yehova huchochea chuki
Kundi la Mashahidi wa yehova lilianzishwa nchini Marekani karne ya 19.
Huwa wanafasiri Biblia moja kwa moja na miongoni mwa mengine waumini wake hawaruhusiwi kutoa au kupokea damu.

Huwa hawatazamwi na makanisa mengine makuu ya zamani ya Kikristo kama madhehemu makuu.

Wakati wa utawala wa Joseph Stalin katika Muungano wa Usovieti, kundi hilo lilipigiwa marufuku na maelfu ya waumini wake wakapelekwa Siberia kuteswa. makundi mengine ya kidini yalihangaishwa na serikali pia.

Muungano wa Usovieti ulipoporomoka, dini za Kikristo zilifufuka Urusi na marufuku dhidi ya Mashahidi wa yehova ikaondolewa mwaka 1991.

Lakini msimamo wa serikali dhidi ya kundi hilo la kidini ulianza kuwa mkali tena na mwaka 2004 lilituhumiwa kwa kuwaandikisha watoto kuwa waumini na pia kuwazuia waumini kupokea usaidizi wa kimatibabu.BBC

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...