Bado tu tukio lililotokea Ujerumani la bomu kulipuka karibia na basi
la klabu ya Borussia Dortmund linaitesa shirikisho la soka barani Ulaya
UEFA.
Sasa kuelekea katika mchezo wa fainali ya Uefa Champions league utakaopigwa mwezi june kati uwanja Principality Stadium,
kumekuwa na hofu kwamba magaidi wanaweza kutumia ndege ndogo za kurusha(drones) kushambulia uwanja huo.
Maofisa wa UEFA wamefanya vikao vya siri na maofisa wa usalama wa Wales na wa uwanja huo ili kujaribu kutafuta mbinu sahihi ambayo itasaidi kudhibiti jambo hilo lisitokee wakati wa fainali hiyo.
UEFA wameanza kufikiria kuuziba uwanja huo kwa juu ili vitu kama drones visiweze kupenya katika uwanja huo kupitia juu, suala ambalo tayari wamiliki wa uwanja huo wameanza kulifanyia kazi.
Fainali hiyo itakayopigwa tarehe 3 June inatarajia kuvuta watu mbali mbali katika kila kona ya dunia,
huku uwanja huo utaweza kubeba watu 75,000 na ujio wa watu wengi siku hiyo inaweza kuwavutia magaidi suala ambalo UEFA wameanza kulihofia.
Inasemekana zaidi ya askari 14,000 tayari wamejipanga kufanya kazi ya ulinzi siku hiyo, huku pia kukianza kufungwa vifaa maalum karibia na uwanja huo ambavyo vitaweza kugundua vitu vya mlipuko.
Kundi la kigaidi la IS(Islamic State) ndio limekuwa likileta hofu kubwa katika soka kwani hata mlipuko uliotokea Dortmund polisi wamekiri kuwa mlipuaji alikuwa mzoefu sana,
na kundi hilo ndio limekuwa likitumia drones mara nyingi katika matukio yao.

Comments
Post a Comment