Skip to main content

PROFESA LIPUMBA ATINGA MAHAKAMANI.!

Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.
 
Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama. 
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.
 
Maombi hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama wakiwa viongozi halali wa chama hicho, wanaomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kwa kuwa wana masilahi na shauri hilo.
 
Wakili wa CUF upande wa Katibu Mkuu, Juma Nassoro na Wakili wa Serikali, Hang Chang’a waliieleza mahakama kuwa bado hawajapewa hati za maombi hayo.
 
Jaji Wilfred Dyansobela aliamuru waombaji hao (kina Lipumba) kuwapatia nyaraka hizo na amepanga kusikiliza maombi hayo Juni 6, siku ambayo kesi ya msingi itatajwa.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...