Skip to main content

Zitto Kabwe kuhusu uchaguzi wa ubunge wa EALA kundi la vyama vya upinzani..!


Moja ya habari iliyochukua headlines kwenye magazeti ya leo ni pamoja na kuhusu Zitto Kabwe na CHADEMA kudaiwa kutifuana sababu ikiwa ni uchaguzi wa  ubunge wa Afrika Mashariki ‘EALA’.

 Aidha mijadala mikali imeendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uchaguzi huo kundi la vyama vya Upinzani.
Sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook Kiongozi wa ACT Wazalendo ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameyaandika haya…..
ACT Wazalendo kama chama chenye uwakilishi Bungeni kina haki ya kuweka wagombea na tumeshamteua Prof. Kitila Mkumbo katika nafasi 1 kati ya nafasi 3 za Vyama vya Upinzani.

Ninaamini kuwa nafasi 1 hii kuchukuliwa na Mtanzania wa kaliba ya Prof. Kitila Mkumbo haiwezi kuwa ndio hatma ya Upinzani nchini.
 Eti nafasi moja EALA inayoombwa na ACT Wazalendo kati ya nafasi 3 zilizopo iwe chanzo cha kuvunja Umoja wetu kwenye masuala makubwa ya nchi? We have a war to fight, EALA is just one of the battles. Haiwezi kuwa ndio hatma ya vita kubwa.

Mzee Edward Lowasa hupenda kutumia msemo wa Rais Mstaafu Ahmed Ben Bella wa Algeria ” we have to die a little “. Hekima Hii ni kubwa Sana. 

ACT Wazalendo kupata kiti kimoja EALA kuwakilisha nchi yetu, tena Kwa kupeleka Mtanzania mmoja bora kabisa hauwezi kuwa kikwazo cha Vyama vya Upinzani kufanya kazi pamoja kwenye mambo makubwa zaidi. Kutaka kuzuia ACT Wazalendo kuweka wagombea wa EALA ni kiwango cha juu cha ukiukwaji wa misingi ya Demokrasia.

Tuweke maslahi ya Nchi mbele Kwa kupeleka EALA watu wenye uwezo mkubwa na wasio na mashaka kuhusu uzalendo wao. Kule EALA tunakwenda kupambana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

 Tukiendekeza vyama na kupeleka watu Kwa sababu ya Vyama vyao tu hatuindei haki nchi yetu. Tuache masihara kwenye maslahi ya nchi.

Tunataka mtu ambaye kwenye Tanzania atasema ” Right or Wrong, my country First “. Prof. Kitila Mkumbo ni mtu wa namna hiyo. Akose kuwakilisha nchi Kwa sababu yeye ni ACT Wazalendo? Kosa lake ni kuwa ACT Wazalendo? Kweli?

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...