Skip to main content

Baada ya Diamond, Shigongo amgeukia Alikiba, ampa ushauri huu.!

Baada ya kufunguka mengi kuhusu Diamond na uongozi wake na mwishowe kuambulia matusi ya kila namna kutoka kwa mashabiki wa staa huyo, Eric Shigongo sasa amemgeukia Alikiba na uongozi wake.
Hiki ndicho alichokisema:
Kwanza kabisa nianze kwa kukiri kuwa sikuwahi kukutana na Ali kiba ana kwa ana mpaka miezi miwili iliyopita nikiwa katika Hotel ya Double Tree, iliyopo Masaki, Jijini Dar Es salaam.

Nilikwenda pale kwa ajili ya chakula cha mchana na mke wangu. Muda mfupi tu baada ya sisi kuingia walifika Ali Kiba na Meneja wake Christine Mosha (Seven) wakaja moja kwa moja kwenye kona tuliyokaa na kutusalimia.
Kitu cha kwanza nilichojifunza na kukipenda kwa Ali kiba ni unyenyekevu, kijana huyu ni mnyenyekevu mnoooo! Kitu hiki peke yake ukiachana na muziki wake kilinifanya nimpende Kiba. 

Walipoondoka mimi na mke wangu wote tulikiri KIBA NI MNYEYEKEVU NA NDIYO SABABU AMEFANIKIWA SANA KATIKA MUZIKI.

Tunapoongelea mafanikio ya Kiba kamwe hatuwezi kuacha kumpongeza meneja wake, hongera Seven. Msichana huyu mdogo ni humble, smart, intelligent and clever! Bila Shaka ndiyo siri kubwa ya mafanikio ya Kiba katika muziki. 


Wiki chache baadae Ali kiba alishinda Tuzo ya MTV huko Africa Kusini na kuliletea taifa letu sifa kubwa sana! Sikuwepo uwanja wa ndege wakati wa mapokezi yake lakini Globaltv Online,
                             walitengeneza ‘Documentary’ nzuri sana iliyoonyesha jinsi kijana huyo alipokelewa kifalme na mamia ya vijana, kuliko ambavyo hata timu yetu ya taifa hupokelewa, BRAVO KIBA.

Makundi ya vijana walikuwepo uwanja wa ndege kuonyesha mapenzi yako kwa Kiba, vijana wa kawaida, wanaishi maisha ya kawaida, wafanyabiashara ndogondogo, wanafunzi n.k. Hapakuwa na mfanyakazi wa CRDB, BOT ana Standard Chartered mahali pale! Sikuona aliyefunga tai na shati jeupe mahali pale.

Gari ya Kiba ilisukumwa, vijana wale walijichangisha elfu moja moja mpaka kutimiza pesa ya mafuta ya gari la Kiba! Hakika hii ni ishara ya upendo mkubwa kwa Kiba.


Leo nitamshauri Ali Kiba! Si kila mtu atataka ushauri, si kila mtu anapenda kushauriwa. Hata ukimwambia mlevi acha pombe, atakuchukia, hata ukimwambia mvuta sigara aachane na sigara kwa kuwa inaua, atakuchukia, kuchukiwa ni sehemu ya maisha yetu, haikuanza jana, juzi, na haitoishia kesho, bado itaendelea kuwa hivyo vizazi mpaka vizazi.

 Baada ya kumshauri Diamond leo nataka nimshauri Ali Kiba. Sijui kama atafurahi au atachukia, ninafanya hivi kwa kuwa sitaki waache muziki hapo baadaye huku wakiwa hawana kitu. Sitaki baadaye mtu aseme kwamba kuna watu waliwatumia, wakaingiza pesa halafu wamewakimbia. 

Baada ya kusema hayo hebu niongee kilichonisukuma kuandika hiki ninachokiandika, ni ushauri, Kiba na meneja wake wanaweza kuuchukua ama kuuacha! Si lazima, kama mhamasishaji wa watu kujiondoa katika umasikini ninaona kama ninao wajibu wa kumshauri Kiba nikiwa kama kaka,
 anko au Mtanzania mwenzake,
  naamini kwa hekima walizonazo Ali Kiba na meneja wake bila shaka watapata la kuchukua, yasiyofaa wataniachia mwenyewe.
Nampenda Kiba sana tu na ninajivuna sana kuwa Mtanzania mwenzake na ningependa kuona anafanikiwa zaidi katika kazi yake.
 Kama siwezi kufurahi mafanikio ya Watanzania wenzangu basi hakuna haja ya mimi kuzunguka huku na kule ndani na nje ya nchi yangu kuhubiri injili ya mafanikio, watu watoke kwenye umasikini unaolitesa taifa langu.
 Haikutokea tu Ali kiba akawa anapendwa vile, la hasha, ni matokeo ya vitendo fulani ambavyo amekuwa akivifanya maishani mwake mpaka Akawavuta watu kumpenda! Mambo hayo hayo akiyaacha hata followers wa Instagram wanaomfanya ajisikie anapendwa leo wataondoka!

Ali kiba, meneja wake na Watanzania wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha ulipo.
 Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo ndiyo utakuwa mwisho wako.

Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake.

 Leo ni Kiba kesho atakuwa mwingine, swali la kujiuliza ni kwamba: SIKU ALI KIBA ATAKAPOKUWA NJE NANI ATABAKI NAYE? Sasa hivi gari lake linasukumwa na anazungukwa na watu kila anakokwenda, lakini ipo siku atakuwa si maarufu tena kama ilivyotokea kwa Mr Nice, Inspector Haroun na wengine wengi!

Atafanya Nini kiba siku atakapokuwa anakaa kwenye meza hotelini viti vingine vyote havina watu? Hakuna mpambe? Au Meneja? Haya mambo yatatokea ndugu zangu..

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...