Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2017

KOMBORA JINGINE LA KOREA YA KASKAZINI LAFELI KATIKA MAJARIBIO.Bofya picha hii kusoma yote

Rais wa Marekani Donald Trump ameishtumu Korea kaskazini kwamba imeikosea heshima China, mshirika wake mkuu, kwa kufyatua kombora la tatu katika kipindi cha mwezi mmoja. Kwenye ujumbe wa Twitter, bwana Trump amemsifu rais wa Uchina, Xi Jinping. Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema jaribio hilo lilitibuka, kwani kombora hilo lilianguka punde tu baada ya kupaa angani. katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Rex Tillerson, ameonya kwamba huenda kukaibuka majanga mabaya sana iwapo miradi ya Kim Jong Un ya kutengeneza zana za kinyuklia na makombora ya masafa marefu hiatositishwa. Maafisa wa Marekani wanasema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka. Hii ni ishara kwamba Korea Kaskazini haina ujuzi wa kutosha kiteknolojia, ama pia huenda ikawa Marekani imepata mbinu ya kuingiilia mifumo yake ya teknolojia. Maafisa wakuu wa Korea kusini na Japan wamekashifu vikali majaribio ya hayo. Msemaji wa wizara ya mabo ya nje wa...

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA BASI LA DORTMUND MBARONI UJERUMANI.! Bofya picha hii.

Polisi ya Ujerumani imemtia mbaroni mwanamme Mjerumani mwenye asili ya Urusi,  anayeshukiwa kufanya mashambulizi dhidi ya basi lililokuwa likiwasafirisha wachezaji wa klabu ya Borussia Dortmund wiki iliyopita. Makomando wa polisi ya Ujerumani, kwa niaba ya ofisi mwendesha mashitaka wa shirikisho wamemkamata mtuhumiwa huyo,  mwenye umri wa miaka 28 katika mji wa Tübingen katika jimbo la Kusini Magharibi mwa Ujerumani la Baden Württenberg. Taarifa za awali kutokana na uchunguzi uliofanywa zimeonyesha kuwa mshambuliaji huyo aliyetambulishwa kwa jina la Sergej W. alitaka kunufaika na kuanguka kwa thamani ya hisa za klabu ya Borussia Dortmund, ambako alitarajia kungetokana na taarifa za mashambulizi kwenye basi iliyobeba wachezaji wa klabu hiyo. Uchunguzi umebainisha kuwa Sergej alikuwa amenunua hisa za klabu hiyo zenye thamani ya euro 78,000 kupitia mtandaoni,  akiwa katika hoteli ya klabu hiyo alikokuwa amekodi chumba kuanzia tarehe ...

PROFESA LIPUMBA ATINGA MAHAKAMANI.!

Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.   Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.   Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama.  Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.   Maombi hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama...

MAHAKAMA NCHINI URUSI YAPIGA MARUFUKU MASHAHIDI WA YEHOVA.!

Mahakama ya Juu nchini Urusi imekubali ombi la serikali kuorodhesha kanisa la Mashahidi wa Yehova, kwa Kiingereza Jehovah's Witnesses,  kama kudi la kidini lililoharamishwa, na kuliorodhesha kuwa kundi lenye msimamo mkali. Wizara ya haki nchini humo ilisema kundi hilo lilikuwa limesambaza nyaraka zilizokuwa na ujumbe wa kuchochea chuki dhidi ya makundi mengine. Mawakili waliokuwa wanatetea kundi hilo wamekanusha madai hayo na wamesema watakata rufaa. Kundi hilo la kidini lina waumini 175,000 nchini urusi, taifa ambalo wafuasi wa madhehebu hayo waliteswa na kudhulumiwa wakati wa utawala wa Josef Stalin. Inakadiriwa kwamba kuna watu milioni nane kote duniani ambao ni waumini wa madhehebu hayo ya Kikristo, yanayofahamika sana kwa kampeni zake za kwenda nyumba kwa nyumba kutafuta waumini wapya. Wafuasi wa kundi hilo la kidini wanasema hatua ya kuharamisha kundi hilo ina maana kwamba shughuli zake pia ni haramu kisheria. Wizara ya haki iliiomba mahakama kufu...

MAHAKAMA YATOA AMRI AGNESS MASOGANGE AKAMATWE.!

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili. Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa. Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo. Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange. Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa. Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, a...

MAREKANI: IRAN INAFANYA UCHOKOZI WA HALI YA JUU.!

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameituhumu Iran kwa kufanya "uchokozi wa hali ya juu" unaoendelea ambao amesema unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika kanda hiyo. "Iran isipochukuliwa hatua inaweza kwenda njia sawa na ya Korea Kaskazini na kuubeba ulimwengu wote katika safari hiyo," Bw Tillerson amesema. Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Hata hivyo, Marekani imekiri kwamba Tehran inatii makubaliano hayo ya mwaka 2015. Iran kufikia sasa haijasema lolote kuhusu tamko hilo jipya kutoka kwa Marekani. Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia. Jumanne, Marekani iliituhumu Korea Kaskazini na kusema taifa hilo lilikuwa linajaribu kufanya "uchokozi kutokee jambo fulani", baada ya nchi hiyo kuf...

KOREA YA KASKAZINI INAAMINIKA KUMILIKI SILAHA 1000 ZENYE UWEZO TOFAUTI.!

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani. Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90. Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti. Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi. Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13. Image caption Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho            ...

HII KALI ! KUMBE HADI BBC WANAKOSA HABARI ZA KUTANGAZA.!!

Siku hizi ni vigumu sana kutafakari hali ilivyokuwa kabla ya mafanikio makubwa kupatikana katika teknolojia ya mawasiliano. Imekuwa kama ada kwamba kila wakati lazima kuwe na habari. Lakini zamani, hali ilikuwa tofauti kabisa. Miaka 87 iliyopita, mnamo 18 Aprili 1930, msomaji wa habari katika BBC alikosa cha kutangaza. Taarifa aliyoisoma wakati wa taarifa ya habari ya saa tatu kasorobo usiku ilikuwa: "Hakuna habari". Baadaye, kinanda kilichezwa kwa dakika 15 zilizosalia ambazo zilikuwa zimetengewa habari.  Baadaye, matangazo yalipelekwa Ukumbi wa Malkia katika jumba la Langham Place, London ambapo kulikuwa na tamasha la muziki wa Wagner. Miaka 87 baadaye, hali ni tofauti kabisa. Jumanne ilikuwa siku iliyojaa habari tele. Watu walipokuwa wanashiriki pilkapilka za hapa na pale baada ya Pasaka, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May aliitisha kikao saa tano mchana na kuahidi kutoa tangazo muhimu. Wengi walianza kutafakari tangazo lake lingekuwa nini - hadi...

JIWE KUBWA LAPITA KARIBU NA DUNIA.! Bofya picha hii.

Asteroidi kubwa ambayo inakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa wa Jiwe la Gibraltar imepita salama karibu an Dunia. Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita moja, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano hivi umbali kati ya Dunia na Mwezi. Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004. Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku. Picha za mitambo ya rada zilizopigwa kwa kutumia antena ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) iliyo na urefu wa 70m (230 ft) katika kituo chake California zilionesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano. Asteroidi hiyo iliipita Dunia katika umbali wa kilomita milioni 1.8 (maili 1.1 milioni) saa 13:24 BST mnamo Jumatano, 19 April. Inakadiriwa kwamba jiwe jingine kupita karibu...

UWANJA ITAKAPOPIGWA FAINAL YA UEFA(CARDIFF) KUZIBWA KWA JUU KUHOFIA MAGAIDI.!

Bado tu tukio lililotokea Ujerumani la bomu kulipuka karibia na basi la klabu ya Borussia Dortmund linaitesa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA. Sasa kuelekea katika mchezo wa fainali ya Uefa Champions league utakaopigwa mwezi june kati uwanja Principality Stadium,   kumekuwa na hofu kwamba magaidi wanaweza kutumia ndege ndogo za kurusha(drones) kushambulia uwanja huo. Maofisa wa UEFA wamefanya vikao vya siri na maofisa wa usalama wa Wales na wa uwanja huo ili kujaribu kutafuta mbinu sahihi ambayo itasaidi kudhibiti jambo hilo lisitokee wakati wa fainali hiyo. UEFA wameanza kufikiria kuuziba uwanja huo kwa juu ili vitu kama drones visiweze kupenya katika uwanja huo kupitia juu, suala ambalo tayari wamiliki wa uwanja huo wameanza kulifanyia kazi. Fainali hiyo itakayopigwa tarehe 3 June inatarajia kuvuta watu mbali mbali katika kila kona ya dunia,  huku uwanja huo utaweza kubeba watu 75,000 na ujio wa watu wengi siku hiyo inaweza kuwavutia magai...

ALICHOKISEMA CHEGE KUHUSU MAANA HALISI YA GO DOWN.!

Mastaa Chege na Temba ni kati ya wasanii waliodumu kwa muda mrefu kwenye Bongofleva wakifanya vizuri hata nje ya mipaka ya Tanzania ambapo hivi karibuni wameachia wimbo wa ‘ Go down’  unaofanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki. Licha ya wimbo wa Go down kupendwa sana mashabiki wao, lakini wengi hawaijui maana halisi ya wimbo huo na kwa kulifahamu hilo,     Chege ameeleza maana halisi iliyobeba wimbo huo huku akisema haumuongelei mtu wala upepo wa siasa uliopo, bali ni ngoma ya Chege na Temba  ambayo haihusiani na maisha ya mtu binafsi bali jamii. >>>” Ile ngoma ni kwa watu wote ambao wanaongea sana, so, Go down haihusiani na siasa, ni ngoma ya mapenzi. Haihusiani na maisha yangu, ni ngoma ya Chege na Temba inayozungumzia jamii na siyo mtu binafsi. ” – Chege. Chege pia amegusia sababu za kukaa muda mrefu bila kufanya kazi ya pamoja na Temba na kugusia gharama za show zao akisema: >>>” Ni kweli mashabiki wamewazoea C...

NASUBIRI RIPOTI YA WAFANYAKAZI 9000 WA SERILALI WENYE VYETI FEKI ‘FEKI’ – RAIS MAGUFULI.!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati Jumamosi hii akizindua majengo ya Hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka kwa kusema kuwa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji. Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo. “Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi,” alisema Rais Magufuli Aliongeza, “Kwa hiyo mnaweza kuona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibia 19000, mikopo hewa,  wanafunzi ambao walikuwa ni hewa ni zaidi ya 56000.  Kila mahali unapoenda kuna tatizo lakini ni lazima tuyatatue haya matatizo kwa sababu mlinichagua kwaajili ya matatizo haya,”. Rais amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii na kuiunga mkono serikali katika harakati z...

KOREA KASKAZINI YAONYA KUISHAMBULIA MAREKANI NA MAKOMBORA YA KINYUKILIA.!

Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia. Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo. "tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo. ''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia'. Huku kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia,  Gwaride la Jumamosi ilikuwa fursa kwa bwana Kim kuonyesha uwezo wa kijeshi wa taifa hilo. Vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa vile vilivyotajwa kuwa manuwari za Pukkuksong ,makombora ...

MZOZO WA KIVITA KATI YA KOREA YA KASKAZINI NA MAREKANI WAZIDI KUPAMBA MOTO.! Bofya pich hii...

Mzozo kati ya Marekani na Korea ya kaskazini unazidi makali. Jamhuri ya umma wa china inaonya mzozo huo unaweza kuripuka wakati wowote ule na hakuna atakaeibuka na ushindi. Onyo la waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Wang Yi limefuatia vitisho vya rais wa arekani Donald Trump dhidi ya utawala wa mjini Pyongyang." Majadiliano ndio njia pekee ya kupatikana ufumbuzi" amesema waziri Wang katika mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mwenzake wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema "mzozo wa Korea ya kaskazini utashughulikiwa." Yeyote atakaesababisha mzozo katika rasi ya Korea "atabeba jukumu la kihistoria la yatakayotokea" ameshadidia waziri wa mambo ya nchi za nje wa China.  Katika kadhia ya mradi wa nuklia wa Korea ya kaskazini,"Mshindi hatokuwa yule mwenye kutoa maneno makali au anaetaka kuonyesha misuli". Vita vikiripuka, matokeo yake yatakuwa kuibuka hali ambayo h...

VITABU VYA QUR,AN VYAPATIKANA KATIKA VYOO CHUONI DALLAS MAREKANI.!

Polisi wameanza uchunguzi baada ya nakala za korani kupatikana ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas. Picha kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha vitabu hivyo vikiwa ndani ya vyoo. Polisi wa chuo wanasema kesi hiyo ni ya "kushangaza sana" na "isiyo ya kawaida" kwani chuo hicho kina wanafunzi kutoka makabila na dini mbali mbali. Polisi wanajaribu kumtambua mmoja kati ya watu sita walioonekana wakiingia chooni wakati wa tukio hilo la tarehe 28 mwezi wa Machi. Wachunguzi wamekuwa wakikagua video za CCTV wakiwatafuta waliohusika. Hakuna kitu kilichoguswa katika chumba kimoja ambacho huwa na vitabu vya dini tofauti, kulingana na wachunguzi. Mkuu wa polisi Larry Zacharias aliiambia Dallas Morning News: "Hakuna anayemjua mmiliki wa vitabu hivyo." Mohammad Syed ambaye ni rais wa chama cha wanafunzi wa Kiislamu chuoni aliambia vyombo vya habari tukio hilo ni la "kuhuzunisha kweli na pia linatatiza." ...

WANASAYANSI WAGUNDUA UHAI KATIKA SAYARI YA SATURN.! Bofya picha hii kujua zaidi.

Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.  Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo         yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini,  Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani. Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi. "Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite. "Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC. Bahari iliyopo kwenye Enceladu...

CCM KIRUMBA UMEPEWA HADHI YA KIMATAIFA.!

Uwanja wa CCM Kirumba wa mkoani Mwanza umeidhinishwa na CAF pamoja na FIFA kutumika kwa mechi za kimataifa baada ya kukidhi vigezo na viwango vya kimataifa. Rais wa TFF Jamal Malinzi ametweet kuwapongeza wakazi wa jiji la Mwanza baada ya maofisa wa CAF na FIFA kuupitisha uwanja huo baada ya kumalizika kwa ukaguzi. Yanga walikwama kuutumia uwanja huo kwa mechi yao ya kombe la shirikisho dhidi ya MC Alger kutokana na uwanja huo kutokidhi baadhi ya vigezo. Kabla ya mechi hiyo, Yanga walituma maombi CAF wakitaka kubadili uwanja kutoka uwanja wa taifa kwenda CCM Kirumba lakini baada ya uwanja huo kukaguliwa afisa wa CAFalibaini kasoro kadhaa ambazo aliagiza zifanyiwe kazi kabla ya kuanza kutumiwa kwa mechi za kimataifa. Baada ya marekebisho na ukarabati uliofanywa, sasa uwanja huo utatumika kwa mechi za kimataifa hivyo wakazi wa Mwanza huenda wakaanza kushuhudia michezo ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu pamoja na ile ya timu za taifa.

SADIO MANE NJE MIEZI MIWILI.!!

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, atafanyiwa operesheni ya goti siku ya Jumanne, na atakosa kusakata dimba msimu huu wote. Aliumiza gegedu la goti lake la kushoto, baada ya kugongana na Leighton Baines kwenye mechi yao walioichezea katika uwanja wao wa nyumbani iyoishia 3-1 dhidi ya Everton. Meneja Jurgen Klopp amesema kuwa Mane, mwenye umri wa miaka 25, anahitaji upasuaji, na kufanya kuwa "vigumu kwake kucheza msimu huu". Timu ya Liverpool iko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Premia, huku ikisalia na mechi sita tu. Jeraha hilo litamfanya kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili ijayo. Mane alijiunga na klabu hiyo kwa kima cha Pauni milioni 34 kutoka timu ya Southampton msimu uliopita, na amesakata mechi zote sita za Liverpool msimu huu. Katika mechi hizo, walishinda mchuano mmoja, tatu wakatoka sare na wakapoteza mechi mbili.BBC ...

HII KALI;MKE NA MUME KUTOKA KENYA WAHINDA MBIO ZA PARIS MARATHON.!

Mkenya Paul Lonyangata alipata ushindi mkubwa wa saa 2 dakika 6 na sekunde 10 katika historia yake licha ya kupoteza muda bora. Mpinzani wake pia kutoka Kenya katika mbio hizo Stephen Chebogut alikuwa wa pili kwa muda wa saa 2 dakika 6 na sekunde 56 huku Solomon Yego pia wa Kenya akishikilia nafasi ya tatu katika muda wa saa 2 dakika 7 na sekunde 13. ''Nahisi vyema sasa kwa sababu lengo langu lilikuwa kuja hapa na kuibuka mshindi '',alisema. Huku Paris ikiwa na jua Rionoripo ambaye ni mkewe mshindi wa mbio hizo upande wa wanaume Paul Lonyangata aliibuka mshindi. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 aliweka muda bora wa saa 2 dakika 20 na sekunde 50 na hivyobasi kushinda muda wake binafsi aliouweka kwa zaidi ya dakika 4.  Ushindi wa wanandoa hao ulirudisha tabasamu kwa wanariadha Wakenya baada ya habari za kushangaza kwamba bingwa wa mbio za marathon za Olimpiki upande wa wanawake Jemima Sumgong alipatikana ametumia dawa za kusisimua misul...

WANASAYANSI WANASA PICHA YA NYOTA ZILIZOGONGANA ANGANI.!

Wanasayansi wamerekodi picha za kusisimua zinazoonyesha nyota mbili changa zikigongana na kuharibu mpangilio wao. Nyota hizo ambazo ziko kwenye mkusanyiko wa Orion ziligongana miaka 500 iliyopita na kusababisha vumbi na gesi nyingi kuingia kwenye anga yao.          Wanasayansi wanasema kugongana kwao kulitoa nguvu kiasi kama cha zile zinazoweza kutolewa na jua kwa muda wa miaka milioni kumi. Matukio yaliyojiri yamenakiliwa kwenye jarida la maumbile ya nyota,Nyota hutengezwa wakati wingu kubwa la gesi linapoanza kusambaratika.  Kwa umbali wa miaka iliopita mwanga kutoka duniani, pamoja na nyota changa zilianza kuumbika katika wingu kubwa kwa jina Orion Molecular Cloud 1, (OMC - 1). Mvuto ulileta nyota hizo karibu kwa kasi sana hadi miaka 500 iliyopita, huku mbili kati yazo zikigongana ana kwa ana na kusababisha mlipuko mkubwa uliosambaza gesi na vumbi katika anga kwa kasi kubwa. Timu hiyo ya watafiti pia imegundua habari...

Saudi Arabia kujenga mji mpya wa burudani karibu na Riyadh.!

Saudi Arabia imeanzisha mipango ya kujenga mji wa burudani kando mwa mji wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya Gibraltar. Mji huo ambao utakuwa na ukubwa wa kilomita 334 mraba ambao utakuwa sawa na mji wa Las Vegas, utatoa huduma za kitamaduni, michezo na mambo mengine ya burudani. Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani. Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022. Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin Salman mwaka mmoja ulipita,  una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia kutegemea mafuta kwa taifa hilo. Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa. Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh.BBC

Milipuko yawaua watu 36 kanisani nchini Misri,!

Takriban watu 36 wameuawa nchini Misri kufuatia milipuko iliyolenga waumini wa kanisa la Coptic leo Jumapili. Watu 11 waliuawa wakati mlipuko ulitoke katika kanisa la St Mark's Coptic mjini Alexandria. Pope Tawadros II, ambaye ni mkuu wa kanisa la Coptic alikuwa amehudhuria misa katika kanisa hilo. Watu wengine 25 walikuwa wameuawa mapema katika kanisa la St George's Coptic, mji wa Tanta umbali wa takriban kilomita 130 kusini mashariki. Kwa mujibu wa vyombo vya habari ,Pope Tawadros hakuhumia. Msaidizi wake alisema kuwa shambulizi la Alexandria liliendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga nje ya kanisa. Kundi la Islamic State linasema kuwa ndilo liliendesha mashambulizi hayo. Mwezi Disemba mwaka uliopita, watu 25 waliuawa wakati bomu lilipolipuka katika kanisa la Coptic cathedral mjini Cairo wakati wa sala. Ghasia dhidi ya wakiristo wa Coptic, zimekuwa nyingi miaka ya hivi karibuni, hasa tangu mwaka 2013 wakati jeshi lilipompindua rais aliyekuwa amechagu...

Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege futi 42,0000 angani.! Bofya picha hii

Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana. Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso. Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri. Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua. Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini. Mashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.B...

Taarifa ya Abdi Banda kusimamishwa kucheza ligi kuu Tanzania bara.!

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, ilifanya kikao chake juzi Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao. Kuhusu kupulizwa dawa vyumbani Uwanja wa Kambarage Daktari wa Uwanja wa Kambarage, Dk.  Abel Kimuntu amekataa kuwasilisha taarifa yake kuhusu tuhuma za kupuliziwa dawa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Majimaji katika mechi namba 170 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji Stand United.  Klabu ya Majimaji iliwasilisha malalamiko yake kwa Bodi ya Ligi kuhusu suala hilo. Hivyo, Kamati imeagiza suala la daktari huyo lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya hatua za kinidhamu dhidi yake kutokana na kukataa kutoa ushirikiano kwa mwendeshaji wa Ligi juu ya jambo hilo. Kamati ya Nidhamu inatarajiwa kukaa wakati wowote wiki ijayo. Kuhusu Mchezaji Abdi Banda Mechi namba 194 (Kagera Sugar 2 vs Simba 1). Beki wa Simba, Abdi Banda ...

Mourinho anataka kumrudisha Chicharito Old Trafford?

Toka Javier Hernandez auzwe kwenda Bayern Leverkusen ya nchini Ujerumani,  maisha yake kisoka yamebadilika sana na kasi yake ya ufungaji imekuwa ni kubwa sana kiasi kwamba kila mtu anamzungumzia. Wakati Chicharito akiwa anafunga sana magoli huko aliko, inaonekana tatizo la ufungaji ndani ya United halijapata tiba bado kwani pamoja na kufunga sana lakini Zlatan Ibrahimovich anaongoza kwa kupoteza nafasi. Jose Mourinho analijua hilo na akakiri kwamba kama mtu aina ya Chicharito angekuwepi ndani ya Manchester United, baasi hadi hivi sasa angekuwa ameshafunga magoli zaidi ya 20. Chicharito hakuwa na bahati ndani ya Manchester United lakini bado ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo,  michezo mingi aliyoingia akitokea benchi alifunga magoli muhimu lakini Van Gaal alimuuza huku mashabiki wakiwa bado wanamtaka. “Nataka nikupe mfano, kwa jinsi tunavyocheza mpira na kwa jinsi tunavyoshambulia hadi sasa Chicharito angekuwa na magoli 20 au zaidi hata kama angech...

Coutinho aweka rekodi mpya EPL.!

Stoke City wakiwa uwanjani kwao walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wanakngoza goli moja dhidi ya Liverpool,  lakini sub ya Firminho na Coutinho ilibadilisha hali ya hewa baada ya Coutinho kuwasawazishia Liverpool kabla ya Firminho kufunga bao la pili na mchezo kuifanya Liverpool kumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri. Kabla ya mchezo huo Mbrazil mwingine Juninho ambaye anachezea klabu ya Middlesbrough alikuwa ameshafunga magoli 29 na alikuwa ndio Mbrazil anayeongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi ya Uingereza,  huku wakiwa sawa na kiungo huyo wa Liverpool Phillipe Coutinho ambaye naye alikuwa na magoli 29. Lakini goli la jana la Coutinho dhidi ya Stoke City limemfanya Coutinho kufikisha magoli 30 ambayo yanamfanya kuwa Mbrazil kinara wa magoli katika ligi ya Uingereza.  magoli hayo 30 Coutinho ameyafunga katika michezo 132,akifuatiwa na Juninho ambaye ana magoli 29 katika michezo 125. Kiungo wa zamani wa Chelsea Oscar amba...

Hali sii shwari Real Madrid, wachezaji wamkataa Ronaldo.!

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Real Madrid zinasema hali sii nzuri kwa mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo kwani baadhi ya wachezaji wenzake hawataki acheze. Ripoti zinasema kabla ya mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid, baadhi ya wachezaji wa Real Madrid walimfuata kocha mkuu wa klabu hiyo Zinedine Zidane na kumuomba Ronaldo asicheze katika mchezo huo. Inadaiwa Gareth Bale ndio aliongoza kundi hilo la wachezaji wa Real Madrid waliomfuata Zidane huku pia wachezaji wengine akiwemo Luka Modric na kiungo wa timu hiyo Toni Kroos nao walikuwa pamoja na Bale kujaribu kumuomba Zidane asimpange Ronaldo. Inadaiwa wachezaji hao wa Real Madrid wamechoshwa na kiwango cha mchezaji huyo, wengi wanaamini Ronaldo kiwango kimeshuka sana na ndio sababu inayopelekea Real Madrid kupata tabu katika mbio za ubingwa. Lakini pia kuna wachezaji wazawa wa Hispania akiwemo Alvaro Moratta nao hawavutiwi na mpango wa Zidane kumuanzisha Ronaldo kila siku huku wenyewe ...