Skip to main content

UKOSEFU WA CHAKULA WAENDELEA KUZITESA BAADHI YA KAYA DODOMA ..............//

Kutokana na kuwepo kwa tatizo la ukame katika mkoa wa Dodoma inadaiwa kuwa limechangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa chakula katika mkoa huo  hali inayosababisha  kusambaratika  kwa baadhi ya  familia zenye kipato cha chini.

Akizungumza na Wandishi wa Habari,Afisa Mazingira Manispaa ya Dodoma   Hapiness Karugaba amesema kuwa  hivi sasa baadhi ya familia  zinaishi katika mazingira magumu  kutokana  na mavuno kidogo, Amesema  kuwa hali hiyo   imesababisha  baadhi ya familia kushindwa   kuhudumia familia kutokana na pato dogo linalopatikana   ikiwemo kuvuna kidogo na kusababisha kuacha familia zao .

dodoma-kk

Nae  Afisa Lishe wa Manispaa ya Dodoma,  Semeni Juma ameeleza uchache wa mavuno unaotokana na ukame husababisha  ukosefu wa lishe bora  kwa wananchi  hali inayopelekea   udumavu wa akili kwa wananchi hususan watoto wadogo  sanjari na   kuelezea mikakati ya serikali katika kupambana hali hiyo.

Baadhi ya wananchi waishio katika Manispaa hiyo ya   Dodoma  mjini wamesema kuwa hali hiyo  inaawaathiri sana  kutokana na kutegema mvua  kwa ajili ya mazao yao sanjari na kusema kuwa  hali hiyo imejitokeza baada ya kuwepo kwa mabadiliko  ya tabia ya nchi, ambapo  mvua hivi sasa katika mkoa huo huchelewa  kunyesha katika mwezi huu wa Novemba  ikiwa ndiyo mwezi  unaotarajiwa  kunyesha mvua .

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...