Skip to main content

Ujumbe wa Baraza la Usalama la UN wasubiriwa mjini Kinshasa ................//

Nchini DRC, ujumbe wa wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwasili Ijumaa hii Novemba 11 mjini Kinshasa hadi Novemba 14.



Lengo la ziara hii ya siku 3 katika mji mkuu wa DRC na katika mji wa Beni kaskazini mwa nchi ni kupunguza joto la kisiasa lililoshuhudiwa wiki za hivi karibuni wakati ambapo unakaribia mwisho wa muhula wa pili wa Joseph Kabila ifikapo mwezi Desemba mwaka, hasa marufuku ya kuandamana katika mji mkuu Kinshasa na kuzimwa kwa mitambo ya RFI tangu siku 6 zilizopita.



Ujumbe wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa, ni ishara kubwa. Hasa katika wakati huu wa mwaka ambapo mabalozi wa Umoja wa Mataifa hawana kawaida ya kusafiri.



Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni njia ya kuonyesha kuwa jumuiya ya kimataifa inaufuatilia mgogoro wa kisiasa nchini DRC kwa umakini, inataka ufumbuzi wa amani upatikane.



Watu wengi wamekua wakijiuliza ni ahadi gani ujumbe huu utapata kutoka pande husika? Hili ni tatizo kubwa kwani nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wote hawakubaliani kuhusu ujumbe watakaowafikishia wahusika.



Kama Marekani, Ufaransa na Uingereza watapendelea kupata ahadi kutoka kwa Joseph Kabila kwamba hatawania katika uchaguzi wa urais, na kwamba uchaguzi huo uahirishwe hadi mwaka 2017, nchi kama Urusi, China wanafikiria kuwa ni kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi iliyohuru. 

 Nchi hizi mbili zinataka kukaribishwa kwa makubaliano ya kisiasa yaliyoafikiwa na kutiliwa sainimjini Kinshasa tarehe 18 Oktoba kati ya serikali na kundi moja la vyama vya upinzani.



Kuna uwezekano kuwa mabalozi wa Umoja wa Mataifa wakajizuia kuchukua hatua kali na kuwataka tu wadau wote nchini DRC kushiriki uchaguzi uliyohusru na wenye uwazi na kujiepusha na machafuko mapya kama yale yaliyotokea mwezi Septemba uliyopita.


Jumamosi Novemba 12, ujumbe wa Baraza la Usalama la wa Mataifa utakutana na Rais Joseph Kabila na Waziri wa Mambo ya Nje Raymond Tshibanda.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...