Pichani
ni Bi Paulina Kulwa (Kulia) akikabidhiwa hundi ya mfano wa Tsh Milioni
100 baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
Hapa
kazi tu ni kaulimbiu inayohamasisha watu kufanya kazi kwa bidii na
kuzingatia fursa mbalimbali zilizopo, usemi huu umetimia kwa Mama
Paulina Kulwa mkazi wa Mwanza baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi
milioni mia moja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania
kwa kushirikiana na Benki ya CBA.
Paulina
alikabidhiwa hundi hiyo katika ofisi za Vodacom jijini mwanza na Meneja
Masoko na huduma za Kifedha Vodacom Tanzania, Noel Mazoya na kusema
lengo la kuanzisha huduma hii ni kuwasaidia Watanzania kuwa na utamaduni
wa kuweka akiba.
Aidha, Bi Kulwa baada ya kukabidhiwa hundi alisema “Namshukuru Mungu na Vodacom kuanzisha huduma hii maana tayari imenifanya kuwa milionea na kuanzisha ajira kwa Watanzania wengine, lakini pia watoto wangu wanaenda shule na nina nyumba”
Naye Mkuu wa kitengo cha masoko Benki ya CBA, Solomon Kawishe alishukuru ushirikiano kati ya Benki yake na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuleta neema kwa Watanzania.
Bi
Paulina Kulwa (Kulia) akiwa na pacha wake katika duka la Vodacom City
Mall jijini Mwanza katika hafla ya kumpongeza na kumkabidhi hundi baada
ya kuibuka mshindi katika promosheni ya Jiongeze na M-Pawa
Mshindi
wa Jiongeze na Mpawa akiwa na maafisa toka Vodacom na CBA katika hafla
fupi ya kumkabidhi mfano wa hundi na kumpongeza. Toka kushoto ni Ayubu
Kalufya Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Meneja Masoko wa huduma za
Kifedha wa Vodacom Noel Mazoya, mshindi wa milioni 100 Bi Paulina Kulwa,
Solomoni Kawiche Mkuu wa masoko - CBA na Eric Luyangi Mkuu wa MPawa -
CBA
Comments
Post a Comment