Kamati ya maafa ya
mkoa wa Kagera imeishapokea zaidi ya shilingi Bilioni 5.4 hadi kufikia
Novemba 10, mwaka huu ambayo ni michango ya wadau mbalimbali ambao ni
pamoja na taasisi binafsi na zile za kiserikali, mashirika ya
kimaifa,nchi marafiki inatotolewa kwa lengo la kukabili maafa ya
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo na kusababisha madhara
makubwa.
Hayo yameelezwa na
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu mbele
ya waandishi wa habari wakati akielezea juhudi za kamati hiyo katika
kukabiliana na madhara ya tetemeko,
amesema kamati hiyo imeishatumia
kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kutokana na michango hiyo kwa ajili
kukarabati miundombinu ambayo imeharibiwa na tetemeko ambayo ni pamoja
na zahanati,vituo vya afya,shule za msingi na sekondari.
Aidha,mkuu huyo wa
mkoa pamoja na kuwapongeza waliochukua hatua ya kujenga upya nyumba zao
ziliharibiwa na tetemeko,amesema kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera iko
kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi maalumu yenye uhitaji yanarejesha
katika hali ya kawaida miundombinu ya nyumba zao za makazi
iliyoharibiwa na tetemeko,
amesema kamati hiyo tayari imeishafanya
makubaliano na Kanisa la Pentekoste ambalo limeahidi kujenga nyumba za
wenye uhitaji kwa awamu mbalimbali ambapo katika awamu ya kwanza kanisa
hilo litajenga nyumba 370.
Nao baadhi ya wazee
na wajane wameonyesha kutoridhishwa na utaratibu unaotumika wa
kuyabainisha makundi yenye uhitaji,wakizungumza wamesema utaratibu wa
kuyabaini makundi hayo kuwa unawabagua baadhi ya waathirika wa tetemeko
wenye uhitaji.
Comments
Post a Comment