Skip to main content

Rais Magufuli aongoza mamia ya Watanzania kuaga mwili wa Samuel Sitta .....Atuma rambirambi kifo cha Mbunge Hafidh Ali Tahir .........//

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani

Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe.
 
 Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. 
Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.

"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016
.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...