Sunday, 20 November 2016.MAHAFALI YA KUMI NAMOJA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI|Arusha Journalism Training college|..
Hayo yamesemwa na meya wa jiji la Arusha Bwana Kalist Lazaro wakati akiwatunuku vyeti wahitimu wa chuo hicho katika mahafali ya kumi na moja yaliyofanyika mapema jana katika ukumbi wa PPS maeneo ya JR Mbauda jijini hapa.
Meya huyo amesema kuwa waandishi wa habari wanatakakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kupaza sauti zao wakiwa kama vioo vya jamii kuitaka serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania juu ya kuwataka wabunge nawao kuongeza viwango vya elimu zao.
.
meya lazaro amewataka wazazi na walezi kutokata tamaa kwa kuwaendeleza watoto wao kwa ngazi nyingine ya kimasomo ila waweze kuwa bora zaidi na kuweza kukabiliana na soko la ajira kwa sasa kitaifa na kimataifa.
Hata hivyo ameongeza kwa kuwataka wahitimu wa ngazi hiyo ya stashada kutokuishia hapo na kuweza kuongeza viwango vya elimu ikiwemo elimu ya degree kama ambavyo wamevyotakiwa na sheria hiyo ili kuweza kupmbana na soko la ajira.
Aidha wahitimu hao wamewashukuru walimu,uongozi wa chuo , wazazi pamoja na wanafunzi wenzao kwa kuwa pamoja nao kwa kipindi chote cha masomo.
Comments
Post a Comment