Inafahamika ndoa yao ilivunjika ni zaidi ya miaka miwili sasa, lakini bado mastaa Wiz Khalifa na Amber Rose hawajasahau kwamba wao ni wazazi na wana mtoto wa kiume.
Jumatano ya wiki hii mastaa hawa walikutana kanisani huko California wakati wa maadhimisho ya siku ya Shukrani wakiwa na mtoto wao Sebastian mwenye miaka mitatu.
Mrembo model Amber Rose
mwenye miaka 33, alionekana mwenye furaha kukutana na baba wa
mwanae, Hip Hop star Wiz Khalifa ambaye alikuwa amembeba Sebastian.
Wawili hawa walianza kudate 2011, wakachumbiana mwaka 2012 na kufunga
ndoa July 8, 2013.

Comments
Post a Comment