Takwimu
zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne barani Afrika kwa kuwa na vifo
vya mama na mtoto huku ikiwa ya sita duniani kwa vifo hivyo hivyo suala
ambalo wadau wa Afya wanaishinikiza Serikali kuwekeza katika huduma za
dharura wakati wa kujifungua.
Akiongea
leo Jijini Dar es salaam, Katika uwasilishwaji wa ripoti ya miradi ya
afya katika Mikoa ya Morogoro, Kigoma na Pwani Mkurugenzi wa shirika la
Thamini Uhai Dk.
Nguke Mwakatundu amesema jitihada za makusudi za ujenzi
wa huduma za dharura karibu na makazi ya watu hasa maeneo ya vijijini
iongezwe ili kutatua changamoto hiyo.
Dk.
Nguke amesema, wakati umefika kwa Serikali kuhakikisha inatekeleza
mipango mbalimbali iliyojiwekea katika kuhakikisha inapunguza vifo vya
mama wakati wa kujifungua kutoka wanawake 332 kufikia idadi ya wastani
ya wanawake 250 kama ilivyo ainisha katika mpango wa maendeleo wa Taifa
ili kujiletea maendeleo.

Naye,
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga ya Afya ya mama na mtoto kutoka Wizara ya
Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dk.
Kaholeth Winani
amesema, Asilimia 15 ya vifo vya mama na mtoto hutokana na matatizo
yasiyo tabirika wakati wa Uzazi hivyo ni jukumu la Jamii kutambua dalili
za hatari na kuwawaisha kina mama kwenye vituo vya Afya kwani asilimia
85 ya wajawazito hujifungua Salama bila matatizo.
Comments
Post a Comment