Mchungaji
wa Kanisa la Pentekoste Ipagala Manispaa ya Dodoma, Joshua Warioba,
anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka na
kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Tukio
hilo linaripotiwa kutokea Machi 2, mwaka huu, majira ya jioni katika
kituo cha chekechea cha Efretha English Medium Pre and Primary School,
kinachomilikiwa na mchungaji huyo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa Mchungaji huyo
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuingilia mtoto huyo kila siku
alipokuwa akienda masomo ya ziada (tuition) na jalada la kesi hiyo lipo
kwa mwanasheria wa serikali ambae muda wowote atapeleka hati ya mashtaka
polisi ili afikishwe mahakamani.
Mama
wa mtoto huyo anasema kuwa alimwandikisha mwanae kusoma chekechea
katika shule ya kanisa hilo Februari 2. Baada ya mdogo wake kuja
nyumbani kwake na kuuliza kama mwanae nae huwa anahudhuria masomo ya
ziada na kujibiwa kuwa hajui kama kuna masomo hayo. Ndipo alipoamua
kufuatilia kwa majirani wengine pia kuubaini ukweli.
Walipomuuliza
mtoto huyo alisema japo kwa woga vitendo alivyokuwa akifanyiwa na
mchungaji huyo. Ndipo walipoweka mtego na kumfuma mchungaji huyo akiwa
na mtoto huyo kwenye chumba huku nguo zake za ndani zikiwa zimeshushwa.
Wananchi walikusanyika wakitaka kumpiga mchungaji huyo lakini aliokolewa na mwanajeshi mmoja na kukimbizwa polisi.
Baada
ya mzazi huyo kufika polisi aliandikiwa mtoto aende kupimwa hospitali
na majibu ya daktari yalionyesha kuwa mtoto ana michubuko. Alipoulizwa
mtoto huyo alisema kuwa mchungaji alikuwa akimbaka kila alipoenda
kusoma.
Kamanda
Mambosasa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto kwenda kusoma masomo ya
ziada (Tuition) pasipo kuwa na uangalizi wa karibu na pia aliitaka jamii
kuendelea kupiga vita dhidhi ya matendo ya udhalilishaji kwa kutoa
taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Comments
Post a Comment