Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza kwamba "haiwezekani" kwake kuwa meneja wa klabu ya Barcelona ya Uhispania.
Hata hivyo, BBC imefahamu kwamba yeye si miongoni mwa wanaotathminiwa kwa ajili ya kupewa kazi hiyo.
"Mimi ni shabiki wa Espanyol - Nafikiri sihitaji kusema sana kuhusu hilo,"
raia huyo wa Argentina alisema, akisisitiza uhasama kati ya Espanyol na majirani zao wa jiji Barcelona.
Pochettino, 45, pia alichezea Espanyol mechi 216.
Katika kikao na wanahabari Alhamisi Pochettino alisema: "Ni kama siku moja, iwapo (mwenyekiti wa Spurs) Daniel Levy atanifuta kazi, haiwezekani kwangu kuwa mkufunzi wa Arsenal."
Taarifa zinasema Spurs walifahamu kuhusu mkutano wa POchettino na rais huyo wa Barca.
Mkufunzi msaidizi wa Barca Juan Carlos Unzue anapigiwa upatu kumrithi Enrique ambaye anaondoka mwisho wa msimu.
Mkufunzi wa Athletic Bilbao Ernesto Valverde pia anaaminika kuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kupewa kazi hiyo.BBC
Comments
Post a Comment