Ukiacha Juventus ambaye hadi sasa katika michezo 33 hakuna mechi
waliyopigwa, kuna timu ambazo msimu huu hawajapoteza mchezo hata mmoja
wa ligi katika uwanja wao wa nyumbani.
1.Tottenham Hotspur.
Katika msimu huu wa ligi hadi sasa Tottenham
wameshacheza michezo 14 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart
Lane.
Hakuna timu ambayo imetembelea uwanja huo na kuondoka na alama zote
3,Hart Lane pamekuwa pagumu sana kwa wapinzani kwani kati ya mechi hizo
14 walizocheza wameshinda michezo 12 na kutoka suluhu miwili.Tottenham
kwa ujumla msimu huu wamefunga magoli 33 na kufungwa 7 tu,wanatafuta
ubingwa wao wa kwanza tangia mwaka 1961.
2.Real Madrid.
Madrid msimu huu pamoja na kwamba kuna kipindi walikuwa
wakipatwa na matokeo yasiyoeleweka lakini nao hawajawahi kifungwa
nyumbani. Katika ligi yao ya nyumbani Real Madrid msimu huu wamepoteza
michezo miwili tu dhidi ya majirani zao Athletico na ule dhidi ya
Sevilla.
Lakini hawajawahi kufungwa wakiwa Santiago Bernabeu kwani
michezo yao 14 waliyocheza uwanjani hapo wameshinda michezo 11 na kusulu
michezo mitatu, na wakiwa wamefunga magoli 36.
3.Juventus.
Uwanja wa nyumbani wa Juventus umekuwa kama Jehannam kwa
timu zinazoenda kupatembelea msimu huu. Katika ligi ya Italia hakuna
timu ambayo imeambulia alama hata moja katika uwanja huo. Juventus
wamechukua alama zote 45 katika michezo 15 waliyocheza uwanjani hapo, na
ni kati ya viwanja vigumu sana kucheza dhidi yao.
Si hivyo tu bali
katika michezo 33 kwa ujumla ya Juventus hawajapoteza mchezo hata mmoja.
4.Bayern Munich.
Allianz Arena napo ni pagumu, uwanja huo wa nyumbani wa
Bayern Munich hawajawahi kuangusha alama 3 katika uwanja huo. Hadi sasa
katika ligi yao ya nyumbani Bayer Munich wameshacheza michezo 12 katika
uwanja huo, kati ya michezo hiyo wameshinda mara 9 huku wakitoka sare
mara 3 na kupata jumla ya magoli 38.Fc Koln,Hoffeinheim na Schalke 04
ndio timu pekee zilizogawana alama na Bayern katika uwanja huo.
5.Borussia Dortmund.
Wapinzani wakubwa wa Bayern Munich katika ligi ya
Ujerumani, Dortmund nao wakiwa Westfalenstadion hawajapoteza mchezo hata
mmoja. Wameshacheza michezo 11 uwanjani hapo na katila michezo hiyo
wameshinda mara 8 huku wakitoka suluhu mara tatu na kufunga jumla ya
magoli 28.
6.PSG.
Miamba ya Ufaransa, wakiwa nyumbani kwao wameshinda kwa
wastani wa 64% na zilizobaki wametoa suluhu. Michezo 14 waliyocheza
wamepata suluhu michezo 5 huku wakishinda michezo 9 kwa idadi ya magoli
28, wakiwa nyumbani kwao wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 5 tu.
Comments
Post a Comment