Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo kwa sasa lakini inakua kwa haraka sana.
Kulingana na utafiti huo Uislamu unakuwa kwa haraka ikilinganishwa na dini nyengine yoyote ile duniani.
Itaipiku dini ya Kikristo ifikiapo 2070 kulingana na makadirio yake na hivyobasi kuwa dini yenye ufuasi mkubwa duniani.
Mwaka 2010 taifa la Indonesia ndilo taifa lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani lakini sasa India huenda ikawa na wafuasi wengi zaidi duniani ifikiapo 2050.
Hatahivyo taifa hilo litakuwa na wafuasi wengi wa dini ya Hindu.
Wanne kati ya Wakristo 10 duniani watakuwa wakiishi katika jangwa la sahara barani Afrika.
Na nchini Marekani mmoja kati ya watu 50 watakuwa Waislamu kufikia 2050.BBC
Comments
Post a Comment