1.Amekuwa nyota kwa kila timu aliyochezea.Toka alipokuwa Leicester
City mchango wake ulikuwa mkubwa sana na kuisaidia Leicester kubeba
ubingwa.Amehamia Chelsea nako ni vivyo hivyo kwanj amewaweka uongozi wa
ligi na amekuwa muhimu sana kwao.
2.Hana makuu.Kante ni mchezaji ambaye nje ya uwanja
utamuona mshamba mshamba,hana mbwembwe za misuko sijui style za
nywele,na anasema yeye baada ya mechi tu hurudi nyumbani kulala.
3.Alivyokuwa mhimili wa Leicester.Kwa timu ya Leicester
kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa ndoto.Hii ni sababu ambayo kila
timu inatamani kuwa na Kante wao,na ndio maana wakati wa usajili timu
mbali mbali zilimpigania Kante.
4.Tabasamu lake.Kante ni mchezaji ambaye ni ngumu sana
kukasirika na muda wote anaonekana na furaha.Wataalamu wa mambo ya soka
wanasema kati ya kitu ambacho mashabiki wengi wanachofurahi kwa Kante
tabsamu ni mojawapo.
5.Bado anakumbuka alipotoka.Baada ya kutoka Leicester
City wengi walidhani ndio mwisho wa Kante na Leicester,lakini Kante bado
ana mapenzi na Leicester.Katika ushindi wao dhidi ya Sevilla, Kante
alikuwepo kuwashangilia Leicester wakitinga robo fainali ya UEFA.
6.Hakumsaliti Ranieri.Kabla ya kocha aliyewapa ubingwa
Leicester City, Claudio Ranieri kutimuliwa kulikuwa na habari kwamba
wachezaji wakubwa walimsaliti. Ryad Mahrez na Jamie Vardy ninmiongoni
mwa majina makubwa ya wasaliti wa Ranieri. Lakini Ngolo Kante alikuwa
swahiba wa Ranieri na hata katika mchezo kati ya Chelsea na Leicester
City walionekana kufurahi pamoja.
7.Yeye utamuona tu uwanjani.Kante ni mtu ambaye hata
shopping huwa haonekani sana. Muda wake mwingi huutumia nyumbani akitoka
nyumbani ni mazoezini akitoka mazoezini ndani kupumzika.
8.Hakuwa gumzo miaka miwili iliyopita.Ni kama zero to
hero,miaka miwili iliyopita hakuna mtu ambaye alikuwa akimzungumzia
Kante. Miaka hiyo Kante alikuwa Cannas hakuwa na jina na hata kwenye
Social medias lakini sasa yuko mdomoni mwa kila mtu.
9.Sio bishoo.Katika umri wake ni dhahiri kwamba
alitakiwa awe bishoo kama Ozil,Pogba au Depay.Lakini Kante sio bishoo
hata kidogo, ukimuangalia maisha yake utagundua anaishi kama mzee wakati
yeye ni kijana.
10.Siku zinavyozidi kwenda ndiyo anakuwa gumzo.Wengine
walidhani baada ya kuondoka Leicester City ingekuwa mwisho wake na
asingeng’ara akiwa na Chelsea.
Lakini msimu huu anaonekana anaenda tena
kutengeneza historia mpya kwa kuwapa ubingwa Chelsea.
Comments
Post a Comment