Manchester United "hawako tayari
kuwa timu babe" kwa sasa na mashabiki wanafaa kusahau ubabe uliokuwa na
timu hiyo enzi za Sir Alex Ferguson, meneja wa sasa Jose Mourinho
ameambia BBC Sport.
United walishinda mataji 13 ya Ligi Kuu ya
Uingereza chini ya Ferguson, lakini Mourinho amesema kwa sasa ni vigumu
kuwa na ubabe wa aina hiyo.Alipoulizwa iwapo anaweza kurejeshea klabu hiyo ukuu wake kama awali, Mreno huyo alijibu:
"Msijaribu kurudi nyuma miaka 10, 20 iliyopita kwa sababu hilo haliwezekani tena.
Mourinho, 54, alitia saini mkataba wa miaka mitatu Mei mwaka jana kuchukua nafasi ya Louis van Gaal, aliyefutwa kazi licha ya kushinda Kombe la FA.
Mashetani hao Wekundu wamemaliza nambari saba, nne na tano misimu mitatu iliyofuata baada ya Ferguson kustaafu.
Msimu huu wamekwama nambari sita tangu tarehe 6 Novemba.
Mourinho haamini wanakaribia kushinda Ligi ya Premia karibu kila mwaka, lakini hataki klabu hiyo ilegee baada ya kushinda Kombe la EFL msimu uliopita.
"Kwa sababu ya sifa za klabu zenyewe, na mimi binafsi, tuko tayari kupigania kila mechi, kila alama. Lakini kuna pengo kubwa kati ya ndoto za jumla za klabu kubwa kama hii na uhalisia."BBC
Comments
Post a Comment