Skip to main content

Babutale amshutumu Shigongo kuwa na hila za kuharibu biashara zake.!

Baada ya Eric Shigongo kuandika barua ndefu ya kumuonya Diamond kuhusiana na jinsi anavyowawekea ngumu waandaji wa show za ndani kwa kuwatoza bei zile zile kama anavyowatoza wa nje ya nchi na kuhusisha uongozi wa WCB.

BabuTale amefunguka mengi huku akimshutumu Shigongo kuwa na hila ya kuharibu biashara zake kupitia magazeti ya Global Publishers. 

 Kupitia Instagram, Tale ameandika:
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…
                   baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako…
                    siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali….
 tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu…
Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazunga eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. 

Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost…

 ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…
hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….

mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…..

tafadhali heshimu heshima yetu kwako…… “Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao. Babutale amejibu.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...