Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2016

Askari polisi 6 wa Kikosi cha Usalama Barabarani Watumbuliwa Kwa Utovu wa Nidhamu ....................////

Askari  polisi sita wa Kikosi cha Usalama Barabarani, wameondolewa baada ya kukiuka taratibu za kazi. Akizungumza na waandishi wa habari  jana, Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni, Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu, alisema askari hao watapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa Kamishna Musilimu, askari hao kutoka katika mikoa mbalimbali nchini, waliondolewa wakati wa ukaguzi wa utendaji wa kazi kwa askari wa kikosi hicho. “Ukaguzi huo ulifanyika nchi nzima katika barabara kuu kufuatia mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini,” alisema kiongozi huyo wa polisi. Aliwataja askari hao kuwa ni D 9363 Sajenti Richard aliyekuwa wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, G 9958 PC, Edward, aliyekuwa eneo la Lilambo mkoani Ruvuma, H 8234 PC Mungwe, aliyekuwa eneo la Tanesco Jimboni, wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma na WP 3058 Koplo Mariam, aliyekuwa eneo la Igurusi, Mbeya. “Askari h...

Nilishawahi kupigwa kariakoo wakijua mimi ni mchawi-Bi Mwenda.................////

Bi Mwenda ni moja kati wa waigizaji wa muda kwenye soko la uigizaji Tanzania tangu anafanya tamthilia mpaka filamu. Mara nyingi tumekuwa tukimuoa akivaa uhusika wa mchawi, mganga ama mama anayejihusisha na imani za kishirikina, hali ambayo imesababisha watu wengine kufikiri kwamba ndivyo alivyo kwenye maisha yake nje ya camera. >>>Mimi huwaga nashangaa jinsi ambavyo ma drector wanavyoniongoza pale, maana mimi ni msanii siwezi kukataa sehemu yoyote kwenda ni kama bakuli kwenye kabati mboga yoyote ile itapakua sana sana ma director wagu ndivyo wananielekezaga hivyo lakini sio mchawi, sina roho mbaya.. >>>Niliwahi kupigwa kipindi cha nyuma ilikuwa mwaka 2005,  nilipigwa nikapigwa kariakoo,sabasaba nilipigwa, kwaajili naelewa kuwa hiyo i kazi yangu, sikuitilia maan sana ani – Bi Mwenda

PICHA 11: Uhusiano wa Wiz Khalifa na Amber Rose umerudi upya?...............//

Inafahamika ndoa yao ilivunjika ni zaidi ya miaka miwili sasa, lakini bado mastaa Wiz Khalifa na Amber Rose hawajasahau kwamba wao ni wazazi na wana mtoto wa kiume.  Jumatano ya wiki hii mastaa hawa walikutana kanisani huko California wakati wa maadhimisho ya siku ya Shukrani wakiwa na mtoto wao Sebastian mwenye miaka mitatu. Mrembo model Amber Rose mwenye miaka 33, alionekana mwenye furaha kukutana na baba wa mwanae, Hip Hop star Wiz Khalifa ambaye alikuwa amembeba Sebastian. Wawili hawa walianza kudate 2011, wakachumbiana mwaka 2012 na kufunga ndoa July 8, 2013.  September 2014 Amber alifungua kesi mahakamani kudai talaka baada ya taarifa zake kwamba amegundua Wiz Khalifa anadate na mfanyakazi wake. Amber Rose aliwahi kuwa mpenzi wa Kanye West miaka ya nyuma kabla ya kukutana na Wiz Khalifa .

Tekno Miles amesaini deal na Sony Music.................////

Tekno Miles msanii kutokea Nigeria  ni miongoni mwa wasanii waliopata mafanikio makubwa,  Tekno  ambae ni mshindi wa tuzo ya MTV Africa Music Awards kama Best Breakthrough Act , Tekno ameingia tena kwenye headlines baada ya kusainiwa kwenye label  ya Sony ambayo inasimamia wasanii wakubwa duniani. Pia  Tekno  alikuwa miongoni mwa wasanii kutokea Nigeria  walioperform kwenye tamasha la Fiesta, November 5 2016 jijini Dar es Salaam   akiwa na  Yemi Alade ,   Unaweza kuitazama video nimekuwekea hapa chini wakati Tekno anasaini mkataba huo.

Sunday, 20 November 2016.MAHAFALI YA KUMI NAMOJA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI|Arusha Journalism Training college|..

   Wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha|Arusha journalism trainig college| wametakiwa kukabiliana na changamoto za ajira nchini ikiwemo sheria iliyopitishwa na      wabunge kwa waandishi wa habari.   Hayo yamesemwa na meya wa jiji la Arusha Bwana Kalist Lazaro wakati akiwatunuku vyeti wahitimu wa chuo hicho katika mahafali ya kumi na moja yaliyofanyika mapema jana katika ukumbi wa PPS maeneo ya JR Mbauda jijini hapa.  Meya huyo amesema  kuwa  waandishi wa habari wanatakakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kupaza sauti zao wakiwa kama vioo vya jamii  kuitaka serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania juu ya kuwataka wabunge nawao kuongeza viwango vya elimu zao. . meya lazaro amewataka wazazi na walezi kutokata tamaa kwa kuwaendeleza watoto wao kwa ngazi nyingine ya kimasomo ila waweze kuwa bora zaidi na kuweza kukabiliana na soko la ajira kwa sasa kitaifa na kimataifa. Ha...

Friday, November 18, 2016 Daktari FEKI anaswa Hospitali ya Rufaa Dodoma.............//

Mkazi wa Area C mjini hapa, Boniface Kigomba amekamatwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akiwa katika harakati za kuwaonyesha wagonjwa kliniki ya wajawazito.  Tukio hilo lilitokea jana na kusababisha wagonjwa, madaktari na wauguzi kukusanyika katika ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kumshuhudia.  Hata hivyo, Polisi aliyekuwa amevalia kiraia alifika hospitalini hapo saa 8:00 mchana na kumfunga pingu Kigomba na kumpeleka kituoni.  Kigomba alikamatwa akiwa na kitambulisho cha uanafunzi cha Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) chenye namba za usajili T/DOM/2014, muhuri wa hospitali hiyo na kitambulisho kinachoonyesha ni muajiriwa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF.  Vitambulisho vingine alivyokutwa navyo ni cha mpigakura, uanachama wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na karatasi zilizokuwa zimeandikwa gharama za matibabu.  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipata malalamiko kutoka...

Friday, November 18, 2016 Mamlaka ya Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli...........//

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.  Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo.  Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi.  Nahodha Mkuu wa TPA, Kapteni Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70 iliyopewa jina la Valeria Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoshusha mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji Mwema, wakati nyingine inayoitwa Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia matishari.  Boti ya MV Valeria Rugaihuruza imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani ...

Friday, November 18, 2016..Umoja wa Ulaya (EU) Wasema Tanzania ina haki kutosaini Mkataba EPA kama Haijaridhika Nao........................//

BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Roeland Van de Geer amesema Tanzania ina haki ya kuamua kutosaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA) hadi itakapojiridhisha manufaa yake. Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu masuala mbalimbali pamoja na kujibu maswali ya wanahabari hao. Akizungumzia suala la Tanzania kutosaini mkataba huo wa EPA, ambao nchi wanachama waliosaini hufanya biashara bila kutoza kodi, Balozi Van de Geer alisema ingawa wasiwasi wa Tanzania kuwa mkataba huo utadhoofisha juhudi za nchi za kufufua viwanda vyake, haoni kama kuna ushindani kwenye hilo. “Ingawa sioni ushindani unaohofiwa na Tanzania kwenye soko la EPA, lakini uamuzi wake wa kutosaini ni haki yao na nisisitize kuwa ni vyema Tanzania isisaini mkataba wowote ambao wana mashaka nao hadi pale watakapojiridhisha umuhimu wake,”  alisema Balozi Van de Geer. A...

Friday, November 18, 2016 Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu..................//

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro, amesema kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua zaidi kwa sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani Dar es salaam. Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm leo asubuhi, Sirro amedai wao kama jeshi la Polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho baki ni Mwanasheria mkuu wa Serikali kuandaa mashtaka kwa Watuhumiwa. “Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasi wasi kama wasi wasi basi unabaki kuwa wasi wasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni, yeye ni mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya. “Lakini kama ana wasi wasi Zaidi yeye ni ki...

Friday, November 18, 2016 Steven Wassira Chali....Ester Bulaya Ashinda Kesi ya Kupinga Ushindi Wake...............//

Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imetoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Spephen Wassira (CCM).    Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, Mkoani Mara. Mahakama hiyo imeeleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo imemthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo. Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wananchi wanne ambao ni wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana. Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakaazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura vis...

WANAFUZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NAUTANGAZAJI{A.J.T.C}ARUSHA KUFANYA MAHAFALI YA KUMALIZA CHUO......//

 17,November,2016. Wanafunzi wanaomaliza masomo katika Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji{ ARUSHA JOURNALISM TRAINIG COLLEGE }wanatarajia kufanya mahafali ya kumi namoja{11} kwa chuo hicho ikiwa nipamoja nakuwaaga wanafunzi hao  chuoni hapo wakiwa wanamliza masomo yao kwa ngazi ya stahahada kama ilivyokawaida ya kila mwaka kwa chuo hicho. Mahafali hiyo ambayo itafanyika katika viwanja vya PPS maeneo ya JR. MBAUDA   natayari maandalizi yakutosha kuelekea hafla hiyo kubwa yameanza kufanyika kikamilifu zaidi. Akizungumza katika eneo la ukumbi wa uwasilishwaji wa vipindi vya radio na television katika chuo hicho mmoja wa wakufunzi chuoni hapo Mwalim ONESMO ELIA MBISE {pichani}amesema wanafunzi hawana budi kufuata sharia za chuo hicho. “ Unapokuwa chuoni unapaswa kutambua wajibu wako kama mwanafunzi ikiwa ni pamoja na kuhudhuria hapa katika eneo hili lakini pia kuhudhuria madarasani ” Aliongeza nakusema Mwalim huyo baada ya tetesi kuzagaa kwa wan...

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAPEWA ONYO KALI .................//

Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu kote nchini wametakiwa kutumia muda mwingi kujisomea na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu , migomo na maandamano yasiyo na tija kwa taifa ambayo yamekuwa yakiwapunguzia ufanisi katika masomo yao. Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda wakati akizungumza na Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwenye kongamano la 3 lililowakutanisha wahitimu wa chuo hicho mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam. Akiwa mgeni rasmi katika kongamano hilo na mmoja wa wahitimu wa siku nyingi wa chuo hicho Kamanda Suzan Kaganda amesema wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu wanapaswa kutambua kuwa elimu wanayoipata katika vyuo hivyo sio kwa ajili ya manufaa yao binafsi bali ni kwa manufaa ya taifa zima hivyo wanatakiwa kuwa makini na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii. “...

TANZANIA YA NNE AFRIKA KWA VIFO VYA MAMA NA MTOTO ..........//

...... Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya 4 barani Afrika kwa kuwa na vifo vya mama na mtoto huku ikiwa ya 6 duniani kwa vifo hivyo hivyo, suala ambalo wadau wa afya wanaishinikiza serikali kuwekeza katika huduma za dharura wakati wa kujifungua Akiongea leo jijini Dar es salaam katika uwasilishwaji wa ripoti ya miradi ya afya katika mikoa ya Morogoro, Kigoma na Pwani Mkurugenzi wa shirika la Thamini Uhai Dkt. Nguke Mwakatundu amesema jitihada za makusudi za ujenzi wa huduma za dharura karibu na makazi ya watu hasa maeneo ya vijijini iongezwe ili kutatua changamoto hiyo. “Nchi inayoongoza kwa vifo hivyo Afrika ni Nigeria, Democratic Republic of Congo, Ethiopia, Tanzania, na nje ya Bara la Afrika ni pamoja na India na Pakistan, kuna nchi nyingine zimeendelea lakini mila na desturi nayo nikikwazo kikubwa katika kuokoa maisha ya mama na mtoto” amesema Dkt. Nguke amesema, wakati umefika kwa serikali kuhakikisha inatekeleza mipango mbalimbali iliyojiweke...

Ujumbe wa Baraza la Usalama la UN wasubiriwa mjini Kinshasa ................//

Nchini DRC, ujumbe wa wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwasili Ijumaa hii Novemba 11 mjini Kinshasa hadi Novemba 14. Lengo la ziara hii ya siku 3 katika mji mkuu wa DRC na katika mji wa Beni kaskazini mwa nchi ni kupunguza joto la kisiasa lililoshuhudiwa wiki za hivi karibuni wakati ambapo unakaribia mwisho wa muhula wa pili wa Joseph Kabila ifikapo mwezi Desemba mwaka, hasa marufuku ya kuandamana katika mji mkuu Kinshasa na kuzimwa kwa mitambo ya RFI tangu siku 6 zilizopita. Ujumbe wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa, ni ishara kubwa. Hasa katika wakati huu wa mwaka ambapo mabalozi wa Umoja wa Mataifa hawana kawaida ya kusafiri. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni njia ya kuonyesha kuwa jumuiya ya kimataifa inaufuatilia mgogoro wa kisiasa nchini DRC kwa umakini, inataka ufumbuzi wa amani upatikane. Watu wengi wamekua wakijiuliza ni ahadi gani ujumbe huu utap...

WAMAREKANI WAZIDI KUANDAMANA KUMPINGA TRUMP/................//

Maandamano ya kumpinga Rais mteule wa Marekani Donald Trump yanaelezwa kuambatana na ghasia huko Portland, Oregon. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katikati ya mji huo ulioko Magharibi mwa taifa hilo huku baadhi wakivunja vioo vya maduka na magari. Polisi wamewashikilia watu 29 kutokana na ghasia hizo. Waandamanaji wengi wao wakiwa vijana wamesema uongozi wa Trump utasababisha mgawanyiko kwa misingi ya rangi na jinsi.

MICHANGO MAAFA YA KAGERA YAFIKIA BILIONI 5.4 ................//

Kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera imeishapokea zaidi ya shilingi Bilioni 5.4 hadi kufikia Novemba 10, mwaka huu ambayo ni michango ya wadau mbalimbali ambao ni pamoja na taasisi binafsi na zile za kiserikali, mashirika ya kimaifa,nchi marafiki inatotolewa kwa lengo la kukabili maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo na kusababisha madhara makubwa. Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea juhudi za kamati hiyo katika kukabiliana na madhara ya tetemeko, amesema kamati hiyo imeishatumia kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kutokana na michango hiyo kwa ajili kukarabati miundombinu ambayo imeharibiwa na tetemeko ambayo ni pamoja na zahanati,vituo vya afya,shule za msingi na sekondari. Aidha,mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuwapongeza waliochukua hatua ya kujenga upya nyumba zao ziliharibiwa na tetemeko,amesema kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera iko kwenye mchakato wa kuhaki...

SERIKALI IMETAKIWA KUWEKEZA KATIKA HUDUMA ZA DHARURA ..............//

Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne barani Afrika kwa kuwa na vifo vya mama na mtoto huku ikiwa ya sita duniani kwa vifo hivyo hivyo suala ambalo wadau wa Afya wanaishinikiza Serikali kuwekeza katika huduma za dharura wakati wa kujifungua. Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Katika uwasilishwaji wa ripoti ya miradi ya afya katika Mikoa ya Morogoro, Kigoma na Pwani Mkurugenzi wa shirika la Thamini Uhai Dk.  Nguke Mwakatundu amesema jitihada za makusudi za ujenzi wa huduma za dharura karibu na makazi ya watu hasa maeneo ya vijijini iongezwe ili kutatua changamoto hiyo. Dk. Nguke amesema, wakati umefika kwa Serikali kuhakikisha inatekeleza mipango mbalimbali iliyojiwekea katika kuhakikisha inapunguza vifo vya mama wakati wa kujifungua kutoka wanawake 332 kufikia idadi ya wastani ya wanawake 250 kama ilivyo ainisha katika mpango wa maendeleo wa Taifa ili kujiletea maendeleo. Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kinga ya Afya ya mama na mtoto kuto...