Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2017

Mahakama ya Kenya yazuia kuajiriwa kwa madaktari 500 toka Tanzania.!

Madaktari nchini Kenya, wamefanikiwa kuishawishi mahakama nchini humo kuzuia kuajiriwa kwa madaktari 500 kutoka Tanzania. Madaktari hao walienda mahakamani kuizuia serikali ya nchi hiyo kutoa ajira hizo wakidai kuwa kuna madaktari 1,400 wasio na ajira nchini humo.  Wamelalamika kuwa itakuwa ni ufujaji wa fedha kuwa na madakrari 500 wa Kitanzania watakaolipwa tshs 360,000 kwa siku. Mahakama ya kazi imetoa agizo hilo Ijumaa jii (March 31), ikisema kuwa litadumu hadi ombi la maofisa wa afya litakaposikilizwa na kuchambuliwa. “That leave is hereby granted…to quash the decision of the government…to hire foreign doctors to be deployed to Kenya,” zimesema nyaraka za mahakama za March 31. Mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa serikali kuwajibu maofisa hao na suala hilo litatajwa April 19. Mwezi huu Rais Dkt John Magufuli alisema kuwa Tanzania itapeleka madaktari 500 kukabiliana na uhaba uliopo na tangazo la nafasi hizo lilitolewa kuwataka wenye sifa kutuma maombi. ...

Mauricio Pochettino: Meneja wa Spurs asema hawezi kuwa mkufunzi Barcelona.!

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza kwamba "haiwezekani" kwake kuwa meneja wa klabu ya Barcelona ya Uhispania. Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Espanyol alikutana na rais wa Barca Josep Maria Bartomeu wiki iliyopita huku uvumi ukiongezeka kwamba huenda akamrithi Luis Enrique. Hata hivyo, BBC imefahamu kwamba yeye si miongoni mwa wanaotathminiwa kwa ajili ya kupewa kazi hiyo. "Mimi ni shabiki wa Espanyol - Nafikiri sihitaji kusema sana kuhusu hilo,"   raia huyo wa Argentina alisema, akisisitiza uhasama kati ya Espanyol na majirani zao wa jiji Barcelona. Pochettino, 45, pia alichezea Espanyol mechi 216. Katika kikao na wanahabari Alhamisi Pochettino alisema: "Ni kama siku moja, iwapo (mwenyekiti wa Spurs) Daniel Levy atanifuta kazi, haiwezekani kwangu kuwa mkufunzi wa Arsenal." Taarifa zinasema Spurs walifahamu kuhusu mkutano wa POchettino na rais huyo wa Barca. Mkufunzi msaidizi wa Barca Juan Carlos Unzue anapigiwa ...

Babutale amshutumu Shigongo kuwa na hila za kuharibu biashara zake.!

Baada ya Eric Shigongo kuandika barua ndefu ya kumuonya Diamond kuhusiana na jinsi anavyowawekea ngumu waandaji wa show za ndani kwa kuwatoza bei zile zile kama anavyowatoza wa nje ya nchi na kuhusisha uongozi wa WCB. BabuTale amefunguka mengi huku akimshutumu Shigongo kuwa na hila ya kuharibu biashara zake kupitia magazeti ya Global Publishers.    Kupitia Instagram, Tale ameandika: Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…                    baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako…                     siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina bu...

Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza milioni 100 show za ndani ‘ukimya wake bila shoo nyumbani utamzamisha’.!

Eric Shigongo, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amelalamika kitendo cha Diamond kuwatoza mapromota wa nyumbani kiwango kile kile anachowatandika wale wa nje.  Shigongo ni mmoja wa waandaji wakubwa wa matamasha kupitia ukumbi wake wa Dar Live na huenda miaka ya hivi karibuni ameshindwa kuzimudu gharama za kumchukua kutumbuiza. Kupitia Instagram, haya ndio mambo aliyoandika: Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma, aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo. Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya. Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno. Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo ka...

Polisi waanza kumsaka aliyemtolea bastola Mheshimiwa Nape.!

Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kumsaka mtu aliyemtolea bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, NapeNauye. Hayo yalisemwa Ijumaa hii na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso. Awali, Gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba. Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba. “Sisi tumepokea maelezo ya waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi, hilo ndilo ninaloweza kukwambia,” alisema. Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya polisi aliyevalia kiraia kumtishia bastola, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM).   Sambamba na hayo Waziri Nchemba alilaani kitendo hicho na kumuagiza Mkuu wa ...

March 18, 2017 timu ya kwanza imefuzu nusu fainali FA Cup.!

Robo fainali ya kwanza ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) imechezwa kwenye uwanja w Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na kushuhudia wenyeji Kagera Sugar wakipoteza kwa bao 2-1 mbele ya Mbao FC kutoka Mwanza. Mbao walianza kupata bao lao la kwanza kipindi cha kwanza likifungwa na Salum Idd kwa shuti kali la mita 29 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Kagera Sugar Juma Kaseja. Kipindi cha pili Kagera Sugar wakarudi kwa kasi na kulishambulia goli la Mbao wakitafuta bao la kusawazisha, wakati wakiwa katika harakati za kupata goli, Mbao wakafanya shumbulizi la kustukiza lililowapa bao la pili ambalo lilijazwa kambani na Dickson Ambundo aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi. Muda ukiwa unayoyoma, Kagera walifanikiwa kupata gili la kufutia machozi likifungwa na Ame Ally ‘Zungu’ akiunganisha kwa shuti mpira uliopigwa na Mohamed Faki. Mbao FC inakua timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya FA Cup msimu huu ikisubiri kucheza na timu zitakazo ...

Mke wa Michael Essien anunua klabu Itali..!

Mke wa aliyekuwa mchezaji wa Ghana Michael Essien ameinunua klabu ya ligi ya tatu Como ,kulingana na klabu hiyo. Akosua Puni Essien ameripotiwa kulipa pauni 206,000 katika mnada wa klabu hiyo iliofilisika. Mmiliki mpya na timu yake sasa ana mpangowa kuimarisha kikosi cha kwanza pamoja na ile timu ya vijana kukuwa. Wataweka juhudi za kuifanya kurudi katika Serie B na kukuza vipaji vya vijana waliomo. Puni Essien amejielezea kuwa mfanyibiashara ,mshauri, mtu anayependa kusaidia na mama wa watoto watatu. Como imeshiriki mara kadhaa katika ligi ya daraja la kwanza ya Seria A ,ikiwa imecheza sana kati ya 1984 hadi 1989 na hivi majuzi ikiwa 2002-2003 ambapo walishushwa daraja baada ya msimu mmoja. Walishushwa daraja hadi ligi ya daraja la tano baada kufilisika.BBC

Hizi ni sababu 10 kwanini Kante anapendwa na kila mtu.!

1.Amekuwa nyota kwa kila timu aliyochezea.Toka alipokuwa Leicester City mchango wake ulikuwa mkubwa sana na kuisaidia Leicester kubeba ubingwa.Amehamia Chelsea nako ni vivyo hivyo kwanj amewaweka uongozi wa ligi na amekuwa muhimu sana kwao. 2.Hana makuu.Kante ni mchezaji ambaye nje ya uwanja utamuona mshamba mshamba,hana mbwembwe za misuko sijui style za nywele,na anasema yeye baada ya mechi tu hurudi nyumbani kulala.   3.Alivyokuwa mhimili wa Leicester.Kwa timu ya Leicester kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa ndoto.Hii ni sababu ambayo kila timu inatamani kuwa na Kante wao,na ndio maana wakati wa usajili timu mbali mbali zilimpigania Kante.   4.Tabasamu lake.Kante ni mchezaji ambaye ni ngumu sana kukasirika na muda wote anaonekana na furaha.Wataalamu wa mambo ya soka wanasema kati ya kitu ambacho mashabiki wengi wanachofurahi kwa Kante tabsamu ni mojawapo.   5.Bado anakumbuka alipotoka.Baada ya kutoka Leicester City wengi walidhani ...

Arsenal yatwangwa na West Brom Albion.!!

Arsenal ilipata pigo la nne katika mechi tano za ligi baada ya mabao mawili ya Craig Dawson kuisaidia West Bromwhich Albion kuilaza timu hiyo ya Arsene Wenger kwa mabao 3-1. Dawson alitumia fursa ya makosa yaliofanywa na walinda lango la Arsenal kufunga mabao yake yote mawili kwa kichwa kupitia kona zilizopigwa na hivyobasi kuathiri uwezo wa Arsenal wa kumaliza katika timu nne bora. Awali Arsenal ilikuwa imejikakamua baada ya kuwa bao moja chini ,na kusawazisha kupitia Alexi Sanchez likiwa bao la 18 la mchezaji huyo wa Chile msimu huu. Hatahivyo walisalia nyuma kwa mara ya pili dakika kumi za kipindi cha pili baada ya mchezaji wa ziada Hal Robson Kanu kufunga bao, dakika mbili tu baada ya kuingia. Arsenal ambayo ilimpoteza kipa Petr Cech kupitia jeraha walikabiliwa na kutawaliwa na kushindwa kupata bao la pili. Na mwisho wamechi hiyo mashabiki wa timu ya Arsenal waliendelea jitihada za za kumtaka kocha wa klabu hiyo kufutwa kazi kwa matokeo mabaya. Walibeba ...

Tanzania kuisaidia Kenya na madaktari.!

Serikali ya Tanzania imekubali ombi la Kenya la kuisaidia nchi hiyo na madaktari 500 watakaosaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba kufuatia kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo. Rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kenya wa maafisa wa afya uliotumwa kwake na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Kiongozi huyo amesema kuwa Tanzania imekubali ombi hilo kwa kuwa Kenya ni jirani ,ndugu na rafiki wa kweli wa Tanzania na amemtaka waziri wa afya nchini humo Ummy Mwalimu kuharakisha mchakato huo ili maafisa hao waelekee Kenya kutekeleza jukumu hilo. Serikali ya Tanzania imekubali ombi la Kenya la kuisaidia nchi hiyo na madaktari 500 watakaosaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba kufuatia kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo. Rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao baada ya kufanya...

Yanga imeshindwa kusonga mbele michuano ya mabingwa Afrika..!!

Dakika 90 za mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika kati ya Zanaco FC dhidi ya Yanga zimemalizika bila timu hizo kufungana na moja kwa moja Yanga imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.  Yanga imehukumiwa baada ya kuruhusu kufungwa goli kwenye uwanja wake wa nyumbani ambapo ililazimishwa sare ya goli 1-1 kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.  Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuangukia kwenye michuano ya Confederation Cup na kuiacha Zanaco ikifuzu katika hatua ya makundi ya Caf Champions League 2017.  Msimu uliopita Yanga ikiwa chini ya Hans van der Pluijm, ilifuzu hatua ya makundi ya michuano ya Confederation Cup baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Caf Champions League.  Yanga ilihitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili isonge mbele kwenye hatua inayofata lakini imeshindwa kufanya hivyo na kujikuta ikiondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya sare tasa kwenye mechi ya marudiano. ...

Hawa hawajafungwa kwao msimu huu.!

Ukiacha Juventus ambaye hadi sasa katika michezo 33 hakuna mechi waliyopigwa, kuna timu ambazo msimu huu hawajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi katika uwanja wao wa nyumbani. 1.Tottenham Hotspur. Katika msimu huu wa ligi hadi sasa Tottenham wameshacheza michezo 14 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane.   Hakuna timu ambayo imetembelea uwanja huo na kuondoka na alama zote 3,Hart Lane pamekuwa pagumu sana kwa wapinzani kwani kati ya mechi hizo 14 walizocheza wameshinda michezo 12 na kutoka suluhu miwili.Tottenham kwa ujumla msimu huu wamefunga magoli 33 na kufungwa 7 tu,wanatafuta ubingwa wao wa kwanza tangia mwaka 1961.   2.Real Madrid. Madrid msimu huu pamoja na kwamba kuna kipindi walikuwa wakipatwa na matokeo yasiyoeleweka lakini nao hawajawahi kifungwa nyumbani. Katika ligi yao ya nyumbani Real Madrid msimu huu wamepoteza michezo miwili tu dhidi ya majirani zao Athletico na ule dhidi ya Sevilla.    Lakini hawajawahi ...

Ndege zagongana hewani nchini Canada.!

Umeshawahi kuskia hii ! Ndege mbili zimegongana zilipokuwa katika anga ya eneo moja la shughuli nyingi za kibiashara huko nchini Canada. Rubani mmoja amefariki na mwengine kureruhiwa vibaya sana. Police wanasema hata ni miujiza kwamba hamna mtu mengine yeyote aliyejurihiwa licha ya ndege moja ya hizo kuanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa la eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal; Ndege nyengine ilianguka eneo la kuogesha magari. Ndege zote ni za aina ya Cessnas kutoka shule moja ya ufunzi wa urubani - Hali mbaya ya hewa ndio inadhaniwa kusababisha ajali hiyo.

Mchungaji Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumbaka na Kumlawiti Mtoto .!

Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ipagala Manispaa ya Dodoma, Joshua Warioba, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano. Tukio hilo linaripotiwa kutokea Machi 2, mwaka huu, majira ya jioni katika kituo cha chekechea cha Efretha English Medium Pre and Primary School, kinachomilikiwa na mchungaji huyo. Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa Mchungaji huyo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuingilia mtoto huyo kila siku alipokuwa akienda masomo ya ziada (tuition) na jalada la kesi hiyo lipo kwa mwanasheria wa serikali ambae muda wowote atapeleka hati ya mashtaka polisi ili afikishwe mahakamani. Mama wa mtoto huyo anasema kuwa alimwandikisha mwanae kusoma chekechea katika shule ya kanisa hilo Februari 2. Baada ya mdogo wake kuja nyumbani kwake na kuuliza kama mwanae nae huwa anahudhuria masomo ya ziada na kujibiwa kuwa hajui kama kuna masomo hayo. Ndipo alipo...

Tundu Lissu afikishwa mahakamani ......Asomewa mashitaka Matano na Kuachiwa Kwa Dhamana .!

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano. Lissu amesomewa Mashitaka matano(5)  ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani,Zanzibar. Serikali imesema upelelezi umekamilika na   ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo.Lissu aliiomba mahakama isisikilize  kesi hii  leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha. Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

Lowassa amtaka Rais Dkt Magufuli kufuta kauli yake..!

Aliyekuwa Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, amemtaka Rais Dkt. John Magufuli kuifuta kauli yake ya kuwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasishirikiane na wabunge wa vyama vya upinzani. Alizungumza hayo jana kwenye ziara ya viongozi wa CHADEMA katika mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Lowassa alidai kuwa kauli hiyo ya Rais Dkt. Magufuli inabomoa misingi ya amani iliyowekwa na waasisi wa taifa letu.  Alisema “Namuomba Rais aisahihishe kauli hiyo na nawaomba watanzania tukatae kugawanywa… Tusikuballi, nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa. Ikienda vibaya tutaangamia wote na ikienda vizuri tutafaidi wote, kwahiyo tukatae. ” Aliongeza kuwa watanzania wamekuwa wakiishi bila kubaguana kwa misingi ya dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka kuiacha. Katika kikao hicho alizungumzia pia juu ya hali ya m...

Dini ya Kiislamu kuipiku ile ya Kikristo kwa ukubwa 2070..!

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo kwa sasa lakini inakua kwa haraka sana. Hata hivyo hilo huenda likabadilika iwapo mwenendo wa watu wanaojiunga na dini hiyo utaendelea, kulingana na utafiti uliochapishwa na kituo cha utafiti cha Marekani Pew Research Center. Kulingana na utafiti huo Uislamu unakuwa kwa haraka ikilinganishwa na dini nyengine yoyote ile duniani. Itaipiku dini ya Kikristo ifikiapo 2070 kulingana na makadirio yake na hivyobasi kuwa dini yenye ufuasi mkubwa duniani. Mwaka 2010 taifa la Indonesia ndilo taifa lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani lakini sasa India huenda ikawa na wafuasi wengi zaidi duniani ifikiapo 2050.  Hatahivyo taifa hilo litakuwa na wafuasi wengi wa dini ya Hindu. Idadi ya Wakristo nchini Uingereza na Ufaransa itashuka kwa asilimia 50 na asilimia 10 ya watu wanaoishi Ulaya wanakadiriwa kuwa Waislamu kufikia 2050. Wanne kati ya Wakrist...

Jose Mourinho: Manchester United hawako tayari kutawala EPL........!

Manchester United "hawako tayari kuwa timu babe" kwa sasa na mashabiki wanafaa kusahau ubabe uliokuwa na timu hiyo enzi za Sir Alex Ferguson, meneja wa sasa Jose Mourinho ameambia BBC Sport. United walishinda mataji 13 ya Ligi Kuu ya Uingereza chini ya Ferguson, lakini Mourinho amesema kwa sasa ni vigumu kuwa na ubabe wa aina hiyo. Alipoulizwa iwapo anaweza kurejeshea klabu hiyo ukuu wake kama awali, Mreno huyo alijibu: "Msijaribu kurudi nyuma miaka 10, 20 iliyopita kwa sababu hilo haliwezekani tena. Mourinho, 54, alitia saini mkataba wa miaka mitatu Mei mwaka jana kuchukua nafasi ya Louis van Gaal, aliyefutwa kazi licha ya kushinda Kombe la FA. Mashetani hao Wekundu wamemaliza nambari saba, nne na tano misimu mitatu iliyofuata baada ya Ferguson kustaafu. Msimu huu wamekwama nambari sita tangu tarehe 6 Novemba. Mourinho haamini wanakaribia kushinda Ligi ya Premia karibu kila mwaka, lakini hataki klabu hiyo ilegee baada ya kushinda Kombe la EFL ms...

Robo fainali ya Ligi ya mabingwa Waulaya rasmi hadharani......!!!

Hatimae robo fainali ya michuano ya Champions leauge imewekwa hadharani,baada ya timu 8 kufudhu sasa zitapambana kwenye wiki ya tarehe 10 April ili kutafuta timu zitakazocheza nusu fainali ya champions league. Mabingwa watetezj wa ligi kuu Uingereza timu ya Leicester City baada ya kuwatoa Valencia sasa watapambana na Athletico Madrid,Athletico wana njaaa na ubingwa safari hii baada ya kupoteza katika fainali iliyopita ya Champions League.Leicester hii sio mara yao ya kwanza kukutana na Athletico kwani wameshakutana mara mbili hapo kabla ikiwa ni mwaka 1962 na 1998 huku Leicester akipoteza michezo yote miwili. Miamba ya Ujerumani Borrusia Dortmund nao watakuwa wenyeji wa Monaco ambao waliitoa Man City katika mechi za 16 bora.Dortmund wenyewe walifudhu katika hatua hii baada ya kuwatupa nje klabu ya Benfica ya Ureno.   Mechi kali itakayovuta hisia za watu ni kati ya mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich ambao watacheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya klabu...