Vitendo vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi nchini katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambapo zaidi ya watoto 2,570 wa kike na kiume wamelawitiwa na kubakwa. Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yaliyofanyika jana katika Makao makuu ya watoto yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Helen Kijo-Bisimba alisema idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na ya mwaka jana. Hata hivyo, Mama Bisimba alisema kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, takwimu hizo zinaweza kuwa ndogo kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ulawiti kwa watoto kutoripotiwa polisi kwa sababu ya mila na desturi za maeneo mengi nchini. “Ripoti ya Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kati ya Januari na Machi 2016 inaonyesha matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa yakiendelea kuongezeka kutoka 180 hadi 1765 hayo ni matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo mbalimbali v...