Skip to main content

YANGA WANAHITAJI ALAMA TATU(3) TU KUTANGAZA UBINGWA-VPL .!

Yanga wanahitaji pointi tatu pekee ili kutangaza ubingwa wao katika msimu huu kabla ya mechi za mwisho za ligi Mei 20, 2017. 

Baada ya ushindi wa jana Mei 13, 2017  wa magoli 2-1 dhidi ya Mbeya City, Yanga imefikisha pointi 65 sawa na Simba na inaongoza ligi kutoka na wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Kama watapata pointi tatu kwenye mechi yao ya kiporo itakayochezwaJumanne dhidi ya Toto Africans zitaifanya Yanga kutangaza ubingwa katika msimu huu 2016/2017,

 kwa sababu watafikisha pointi 68 ambapo hata Simba ikishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Mwadui haitasaidia kwa sababu watafikisha pointi 68 sawa na Yanga lakini watahukumiwa na tofauti ya magoli.

Yanga walianza kupata goli la kwanza dakika ya 7 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Simon Msuva ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa krosi ya Hassan Hamisi Ramadhani ‘Kessy’. 

Mbeya City walisawazisha goli hilo dakika ya 58 kupitia kwa Haruna Shamte baada ya kazi kubwa kufanywa na Ditram Nchimbi kisha kumaliziwa na Shamte.

Obrey Chirwa ameendelea kuonesha ubora wake kwenye ligi ya Bongo baada ya kuifungia Yanga goli muhimu ambalo limeamua mchezo wa leo na kuirejesha timu yake kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa VPL.

Chirwa amefunga goli hilo akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Juma Abdul.

Yanga inaizidi Simba kwa wastani wa magoli 11, Yanga ina wastani wa magoli 43 wakati Simba wao wanawastani wa magoli 32 hadi sasa.

Simba imebakiza mechi moja ili imalize mechi zake zote (30) za ligi kuu Tanzania bara kwa msimu huu, endapo watashinda mechi hiyo watafikisha pointi 68,

 lakini Yanga wamebakiza mechi mbili (Yanga vs Toto Africans na Mbao FC vs Yanga) wakishinda mechi yao ya dhidi ya Toto watatangazwa rasmi kama mabingwa wapya wa VPL matokeo tofauti na ushindi, yatapelekea bingwa kujulikana siku ya mwisho ya mechi za kufungia ligi.

Ikiwa Simba itafungwa kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui basi Yanga watakuwa mabingwa hata kama watapoteza mechi zao zote mbili za mwisho.

Ushindi wa Yanga kwa jana ni sawa na kulipa kisasi kwa Mbeya City kwa sababu mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa November 2, 2016 Mbeya City walishinda kwa magoli 2-1 mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana
Kagera Sugar 2-1 Mbao FC
JKT Ruvu 0-1 Majimaji
Tanzania Prisons 2-1 Ndanda FC
Mtibwa Sugar 4 -2 Mwadui FC

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...