Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amemaliza ziara yake katika ofisi za Shirika la Utangazaji la TBC leo jioni ambapo amelitaka Shirika hilo kuendana na wakati na kuacha mfumo wa kizamani.
Rais Magufuli akipokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Mwakyembe alipotembelea ofisi za TBC .
“Msemaji mkuu wa Serikali ni TBC1 na Redio ya Taifa, kazi yenu ni kutoa taarifa bila kubagua vyama vyao,bila kubagua dini zao, au makabila yao“Alisema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewasifia TBC kuwa wanajitahidi kutafuta habari mpaka za vijijini ila tatizo lao kubwa ni kushindwa kuendana na wakati kwenye matangazo yao.
“Mimi bahati nzuri ni shabiki mzuri sana wa TBC lakini problem yenu mnashindwa kuendana na wakati wa sasa“Alisema Rais Magufuli .
Rais Magufuli amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za TBC leo asubuhi na kuzungumza na uongozi wa TBC pamoja na kusikiliza kero za wafanyakazi.
Comments
Post a Comment