Skip to main content

HAZARD AMEWATABIRIA WACHEZAJI WATATU(3) KUFANYA MAKUBWA KULIKO MESSI NA RONALDO.!

Mshambuliaji nyota wa Chelsea Eden Hazard anatajwa kama mchezaji bora nyuma ya Messi, Ronaldo na Griezman kutokana na kiwango bora anachoonesha akiwa na Chelsea.

Lakini Hazard naye ana maoni yake kuhusu ubora wa wachezaji wengine ambapo anaamini kuna wachezaji bora kuliko yeye na ambao wanaweza kuja kukaa juu ya Messi na Ronaldo.

Lakini ni kama Hazard anaona Messi na Ronaldo wameshindikana kwa sasa kwani anaona wachezaji watakaokuwa juu ya Messi na Ronaldo itawabidi wasubirie Messi na Ronaldo wastaafu.

Lakini Eden Hazard ni kama hajaona mchezaji yoyote katika ligi kuu ya EPL ambaye anaweza kukaa juu ya wafalme hao kwaninwachezaji wote aliowataja wanatokea katika ligi zingine.

Hazard katika orodha ya wachezaji watatu ambao anaamini wanaweza kuchukua nafasi ya Messi na Ronaldo amewataja Paulo Dyabala, Antoine Griezman na Neymar kuwa hawa ndio balaa jipya baada ya Messi na Ronaldo.

“Kwa sasa Messi na Ronaldo hakika ni bora(Hasa huyu Messi), lakini wakisataafu yuko Neymar,Dyabala au Griezman wanaweza kufanya waliyoyafanya au hata makubwa zaidi ya hapo” alisema Hazard.

Eden Hazard pamoja na kukosa tuzo yoyote kubwa katila ligi kuu ya Uingereza lakini anaonekana ndio nguzo kubwa kwa Chelsea kubeba ubingwa msimu huu, 
kwa sasa Hazard amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid.

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...