Hakika Paul Pogba amekuwa na msimu mgumu japo kiwango chake uwanjani
sio kibaya sana, lakini nje ya uwanja Pogba amekuwa akipata shinikizo na
presha kubwa toka kwa wadau wa soka.
Dau alilosajiliwa limekuwa gumzo sana na magazeti na wachambuzi wa soka wengi wamekuwa wakimkosoa kutokana na kiwango chake na wengi wakisema ameshindwa kufikia mahitaji ya Manchester United.
Lakini Pogba alitulia, huku msimu ukielekea mwisho Paul Pogba amepatwa na balaa jipya la kuhusu usajili wake kwenda Manchester United ikionekana kulikuwa na ujanja ujanja katika suala hilo.
FIFA inasemekana tayari wameingilia kati suala la uhamisho wa Pogba kwa kuchunguza kiasi kikubwa alichopewa wakala wake Mino Raiola ambaye alikula £41m wakati wa usajili huo.
Maisha ya Pogba wakati yakiendelea kuandamwa na sakata la usajili wa Pogba ghafla kitabu chake cha hadithi ndani ya United kikaaingia tatizo jipya.
Ni kifo cha baba yake mzazi mzee Fassou Antoine ambaye baada ya kuugua kwa muda mrefu hatimaye maradhi yamemchukua akiwa na umri wa miaka 76,
hadi sasa msimu ukielekea mwisho ni wazi kwamba Pogba amekuwa akikumbana na matatizo ndani ya United kuliko wakati yuko Juventus.

Comments
Post a Comment