Skip to main content

KUMBE MAPENZI NI TIBA!! TAFITI ZINAONESHA ;KUFANYA MAPENZI KUNAONGEZA SIKU ZA KUISHI.! Bofya picha hii kujua zaidi.

Amini usiamini Kama wewe ni moja ya watu ambao hufanya mapenzi kwa msimu basi utakuwa upo kwenye hatari ya kupunguza umri wa kuishi duniani, hii ni kwa mujibu wa tafiti.

Watafiti kutoka chuo cha Coventry University cha nchini Uingereza wamebaini kuwa kufanya mapenzi mara kwa mara kwa watu wenye umri kuanzia miaka 28 kwenda juu huimarisha afya zao na kuongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi kikamilifu kuliko wale ambao wanafanya kwa msimu.
Watafiti hao walibaini kuwa watu ambao wanafanya mapenzi mara kwa mara hupunguza msongo wa mawazo hivyo huimarisha afya ya moyo na kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo kama Shinikizo la damu (High Blood Pressure), Koronari za moyo (Coronary Heart Diseases), Mshituko wa moyo (Heart Attack), Peripheral Vascular Disease magonjwa ambayo huwakumba watu wenye umri mkubwa.
Watafiti hao mbali ya kuorodhesha magonjwa ambayo utayaepuka kutokana endambo utafanya mapenzi mara kwa mara wamesema walichukua idadi ya watu 5000 kutoka nchi 10 tofauti tofauti wenye umri kuanzia miaka 50 hadi 80,
 ambapo asilimia 78% kati yao walikiri kuwa hufanya mapenzi kwa wiki mara 5 hadi 6 licha ya kuwa na umri mkubwa.
Asilimia 10% walisema kipindi wakiwa vijana walikuwa wanafanya mapenzi mara 2 kwa siku kabla ya kufikia umri wa miaka 40.
Asilimia 12% walisema hao hufanya mapenzi kawaida kwa wiki mara 1 ingawaje walisema kipindi walivyokuwa vijana walikuwa wanafanya mapenzi mpaka siku mbili tu kwa wiki.
Hata hivyo watafiti hao wamesema asilimia kubwa ya watu ambao hawafanyi mapenzi mara kwa mara wana asilimia kubwa kupata ugonjwa wa Kansa ya tezi dume (Prostate Cancer) wakieleza kuwa Tezi dume huwa zinakua kadri ya umri unavyozidi kuongezeka na huanzia miaka 25,
 kwahiyo kama mwanaume hatajihusisha sana na mapenzi tezi dume zitazalisha wingi wa mbegu na baadae kujaa na kupelekea kuzuia mkojo kutoka vizuri na dalili za ugonjwa huanza kujionesha hata kabla ya kufikisha miaka 50.
Watafiti hao wamesema mapenzi hayo ni lazima yawe salama kwani kuna uwezekano wa kupata magonjwa mengine makubwa endapo wahusika hawatazingatia afya ya miili yao kabla ya kukutana kimwili. 
                  Chanzo: Coventry University

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...