
Jose Mourinho na Baba yake mzazi
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho tayari ameshafika nchini Ureno kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.
Baba yake huyo aitwae Jose Manuel Mourinho Felix 79 amefariki Dunia wikiendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko jijini Setubal nchini Ureno.
Mapema jana Mourinho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole kwa msiba uliompata.
Katika enzi za uhai wake Baba mzazi wa Mourinho alishawahi kuitumikia timu ya taifa ya Ureno na Klabu ya Victoria Setubal FC kwa michezo 250.
Hapa nimekuwekea picha za Mourinho alivyowasili Ureno kwa kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.

Mourinho akipokelewa na baba yake mdogo mapema leo

Mtoto wa kike wa Mourinho wa pili kulia, nae alikuwepo kwenye mapokezi ya baba yake mzazi

Mourinho na Binti yake wakitoka kanisani kwa misa ya marehemu baba yake .

Comments
Post a Comment